Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi(kulia)akiwasili
kwenye makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Arusha,iliyopo wilayani
Arumeru katika ziara yake ya siku tatu na ujumbe wake.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza na
wakazi wa wilaya ya Arumeru kwenye viwanja vya halmashauri ya Arusha
eneo la Sekei,alipata fursa ya kusikiliza kero za mashamba ambayo
aliahidi kuifanyia kazi,kulia ni Mpima Ramani mkoa wa Arusha,Hamduni
Mansoor na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Agatha
Msuya.
Mzee
Alfred Lekshon mkazi wa wilaya ya Arumeru akimweleza Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi jinsi
alivyonyang’anywa shamba lake lenye ukubwa hekari 25.
Mkazi
wa Olosiva ,wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha,ambaye ni mjane
Mwanahamisi Almasi akisimulia kero anazozipata kutoka kwa mtu anayetaka
kumnyang’anya nyumba na kiwanja chake na kuwa amekua akisumbuliwa na
kutishiwa .
Mwekezaji
ambaye kutoka nchini Denmark,Finn Petersen ambaye kutokana na migogoro
ya ardhi ameshindwa kuendelea na uwekezaji wake eneo la Oljoro baada ya
eneo lake kuvamiwa na wananchi.
Mkurugenzi
wa Jiji la Arusha,Juma Idd(katikati)akifafanua jambo wakati akieleza
mpango wa kutekeleza mradi wa kuliweka Jiji la Arusha katika hadhi ya
kimaita utakaotekelezwa hivi karibuni,kulia ni Mpima Ramani wa mkoa wa
Arusha,Hamduni Mansoor.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi(kushoto)akipata
ufafanuzi wa mojawapo wa majalada kwenye ofisi ya Masjala ya Ardhi
kutoka Afisa Ardhi Mteule wa halmashauri ya wilaya ya Arusha,Rehema Mdee
.
Makamu
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Arusha,Agatha Msuya akizungumza
kwenye mkutano wa wananchi kueleza kero za mashamba na viwanja kwa
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Meya
wa Jiji la Arusha,Gaudence Lyimo akizungumza na wananchi kwenye viwanja
vya Makumbusho ya Taifa wakati wa mkutano wa Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi kusikiliza kero za wananchi.Picha
zote na Muungano Saguya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni