Jumanne, 10 Machi 2015

SHANGINGI LA SERIKALI LAPARAMIA UKUTA WA SHULE JIJINI DAR LEO


 Gari ya Serikali aina ya Toyota Land Cruser yenye namba za Usajili STK 7278, ikiwa imeparamia ukuta wa Shule ya msingi Al Muntazir iliyopo kwenye makutano ya barabara ya Sea View na Barack Obama Drive,jijini Dar es salaam,mara baada ya dereva wake (jina kapuni) kushindwa kulimudu gari hilo pale alipochomekewa na gari nyingine ambayo iliingia mitini.ajali hii imetokea jioni ya leo,wakati gari hili likiwa linatokea mjini kuelekea Palm Beach.hakuna aliejeruhiwa katika ajali hii.
Wafanyakazi wa "Break Down" wakiangalia namna ya kuichomoa gari hiyo iliyoparamia ukuta wa Shule ya msingi Al Muntazir iliyopo kwenye makutano ya barabara ya Sea View na Barack Obama Drive,jijini Dar es salaam leo.
Hivi ndivyo ionekanavyo gari hiyo mara baada ya kuchomolewa kwenye ukuta huo.
Mashuhuda wakitazama gari hiyo.
Gari hiyo ikivutwa na "Break Down" mara baada ya kuchomolewa ukutani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa