Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kugonga kokoto
pamoja na akina mama wajasiriamali katika kata ya Elerai mjini Arusha
wakati alipowatembelea na kukagua shughuli zao, ambapo aliwaambia
“Asiwasumbue mtu wala kuwaambieni muondoke kwani ninawafahamu kwa muda
mrefu toka nikiwa Mbunge wa jimbo hili la Arusha mjini miaka ya nyuma”,
aliwaagiza viongozi wa CCM wa kata hiyo kutojiingiza hata kidogo na
kuleta mgogoro na wananchi hao ambao wanajitafutia rizki katika kazi yao
hiyo.
Ameongeza
kuwa CCM ni chama kinachotakiwa kuwasemea na kuwatetea wanyonge na siyo
kuwakandamiza na kuwaonea “Lazima viongozi na watendaji wa serikali na
chama wawajibike kwa wananchi ambao ndiyo walioingia mkataba na CCM
ambayo iliunda serikali inayotekeleza ilani yake” amesema .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya
mkoa wa Arusha akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2010, inayotekelezwa na serikali ya CCM huku akihimiza uhai wa Chama
hicho akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA
NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ARUSHA)Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchimba
mfereji wa kupitisha mabomba ya maji katika mradi wa maji kata ya
Olmot Olkaryan jijini Arusha.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kufungua maji ya bomba katika mradi wa maji kata ya Olmot Olkaryan jijini Arusha.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchimba
mfereji wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Sombetini kwa Mromboo
jijini Arusha.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa
Sombetini kwa Mrombo mara baada ya kukagua barabara hiyo jijini Arusha.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali jijini Arusha.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua shina la wakereketwa la Sakina kwa Shamsi Arusha Raha jijini Arusha.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kushoto akiongozana
na Nape Nnauye na viongozi wa mkoa na wilaya ya Arusha wakati akielekea
kutembelea soko la Kirombero jijini Arusha.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana wakati alipowasili katika soko la Kilombero jijini Arusha.Kada
wa CCM Viola naye akimwaga maneno ya sumu wakati wa mkutano wa katibu
Mkuu wa Ndugu Abdulrahman Kinana na wafanya biashara wa soko la
Kilombero jijini Arusha.Nape Nnauye akizungumza na umati wa wafanyabiashara na baadhi ya wananchi mbele ya jengo la Soko la Kilombero jijini Arusha.Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wakiwa katika mkutano huo.Kiongozi
wa wafanyabiashara wa soko la Kilombero jijini Arusha akisoma risala
kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana huku Nape Nnauye akiwa amemshikia
kipaza sauti.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili katika soko la Kilombero jijini Arusha.Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika
kata ya Remala Arusha kulia ni Diwani wa kata hiyo Bw.Karim Mushi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Maendeleo Group Peter Samwel iliyotolewa na diwani wa kata ya Remala Bw. karim Mushi kulia.Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Maendeleo Group Peter Samwel akijaribu kuendesha pikipiki mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pikipiki hiyo imetolewa kwa kikundi hicho na diwani wa kata ya Remala Bw. Karimu Mushi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni