mkuu wa mkoa akisomewa taarifa na viongozi wa wilaya ya Ludewa
mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Rehema Nchimbi akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Muholo
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya
Wiki ya maji
duniani katika mkoa wa Njombe ilifanyika wilayani Ludewa katika kijiji cha
Muholo kata ya Luana ambapo mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Rehema Nchimbi aliweza
kufanya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji hicho uliojengwa na wafadhiri
kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Ludewa.
Akizindua
maradi huo Dkt.Nchimbi umegharimu kiasi cha shilingi 150 milion aliiagiza
Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kubuni
miradi ya maji ambayo itawasaidia wananchi kwa muda mrefu kwani kwa
kushirikiana na wafadhiri tatizo la ukosefu wa maji safi na salama katika wilaya
linaweza kupungua kama si kuisha kabisa.
Mradi huo
mkubwa uliozinduliwa na mkuu wa mkoa umefadhiriwa na Shirika la Manos Unidas la
nchini Hispania na kutekelezwa na Asasi ya Youth Rural Development Association
(YORDA) ambao unauwezo wa kuwahuduma wananchi wa kijiji hicho kwa zaidi ya
miaka kumi kutokana na uwingi wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni