Jumatatu, 16 Machi 2015

WANANCHI KATIKA KATA YA LUANA WILAYANI LUDEWA KATIKA KATIKA MKOA WA NJOMBE WAMEASWA KUACHA UVIVU NA MANENO BADALA YAKE WASHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO YA KATA YAO CHANGA.

 wananchi wa luana wakifurahia msaada wa vifaa






                   Augustno Lugome agawa vifaa vya michezo wa vijana
HAYA yamesemwa jana na Augustino Lugome mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa na mzaliwa wa kijiji cha Luana alipokwenda kijijini hapo kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati, upatikanaji wa maji safi na salama na elimu.

Aidha aliwataka wazaliwa wa Kata ya Luana wanaoishi nje na ndani ya Ludewa kuangalia walikotoka kwa kushiriki shughuli za maendeleo ili kuwakwamua wazazi wao wanaokabiliwa na wimbi la umaskini wa kipato ikiwemo ukosefu wa mahitaji muhimu kama elimu maji na afya.

Kwa upande wa Afya Lugome alichangia jumla ya mifuko hamsini ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Luana ambayo ujenzi wake ulisimama kwa muda mrefu kwa ukosefu wa saruji huku jengo hilo likijengwa kwa tope hata hivyo nguvu kazi na michango ya wananchi havitoshi kumaliza ujenzi huo.

Katika kijiji cha Muholo Lugome ameshiriki shughuli za maemdeleo kwa  kuchangia jumla ya shilingi milioni nne kwa ajili ya upatikanaji wa maji safi na salama katika kijiji hicho ambacho kwa muda mrefu bila maji.Pamoja na mchango huo Lugome alitoa mchango wa jezi pea mbili Luana, kitongoji cha ituni pea moja, marato jezi seti moja na mipira miwili, mgoholo mpira mmoja, mbwila jezi seti na mipira miwili na kijiji cha muhulo.

Wananchi katika kata hiyo wamefurahishwa na hatua hiyo na kuwataka   vijana wengine kuiga mfano wa kijana huyo hususani katika kusukuma mbele suala zima la maendeleo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa