Ijumaa, 23 Januari 2015

5 BREEKING NEEWS.ASKARI WA JESHI LA POLISI ATOROKA LINDO AMUUA MWANANCHI KW A RISASI WILAYANI LUDEWA.

baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa marehemu.



Askari wa jeshi la Polisi kituo cha Ludewa mjini ambaye alikuwa lindo la bank ya NMB mwenye namba G.6352D/C  aliyefahamika kwa jina moja la Abduel anasadikika kumuua  kwa kumpiga risasi na bunduki aina ya SMG kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la January Mtitu (20) usiku wa kuamkia tarehe 23/01/2015 nyumbani kwa kijana huyo.

Tukio hilo limetokea baada ya Askari huyo kutoroka lindo na kwenda nyumbani kwa marehemu maeneo ya Ludewa mjini mtaa wa Mdonga usiku wa saa sita na kufanya uharifu huo hali ambayo imewashtua wananchi wa mji wa Ludewa ambao hawajawahi kuona matukio kama hayo yakifanyika katika mji wao.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi kutaka kufanya maandamano ya amani kupinga kitendo hicho cha kulaani jeshi la polisi kumuua mwananchi asiye na hatia na pia wamesusia kuchonga sanduku la kuuzika mwili wa marehemu huyo wakitaka jeshi la polisi wilayani Ludewa lihusike katika mazishi ya mwananchi huyo.

Akiongea kwa masikitiko mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni dada wa marehemu January aliyejitambulisha kwa jina la Imani Mtitu alisema marehemu alisikika akibishana na watu katika simu yake ya mkononi kwa muda mrefu majira ya saa sita usiku na baada ya mabishano hayo watu hao walimweleza tunakuja huko kwako  naye akasikika akiwajibu njooni.

Imani alisema Baada ya dakika chache walisikika watu akigonga mlango wa chumba cha kaka yake na kuamua kuuvunja ndipo mabishano yakaendelea huku marehemu akisikika kuwa anasema anaadhibiwa kwa kosa asilolijua ndipo ikasikika sauti ya risasi na marehemu akilalamika kwa uchungu.

Baada ya kukamilisha tukio hilo alisikia vishindo vya watu vikikimbia ndipo alipoamua kufungua mlango wake bila mafanikio kwani ulikuwa umefungwa kwa nje na wauaji hao akaamua kutumia njia ya kutoka dirishani na kwenda katika chumba cha kaka yake ambapo alimkuta akiwa amelala chini na ametapakaa damu,alijaribu kumuuluza ni akina nani waliofanyia tukio hilo hakuweza kujibu kutokana na hali mbaya aliyomkuta nayo ndipo alipoamua kuwaita majirani na kuanza kuwafuatilia wauaji hao ambao walionekana wakikimbia ikiwa moja amevaa sale za jeshi la polisi na mwingine akiwa na mavazi ya kiraia.

“nilisikia wakiongea tunakuua tupo tayari kufukuzwa kazi mara iukasikika mlio wa bunduki katika chumba cha marehemu kaka yangu nilipojaribu kufungua mlango wangu ulikuwa umefungwa kwa nje nakaamua kupitia dirishani na kwenda haraka katika chumba cha kaka na kumuona akiwa tayari hajitambui nikawaita majirani kuwafuatilia wauaji tulifanyikwa kuwaona watu wawili mmoja amevaa nguo za polisi na mwingine nguo za kawaida wakikimbia”,alisema Imani.

Alipo ulizwa mkuu wa wilaya ya Ludewa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Bw.Juma Solomon Madaha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutuliza jazba kwani bado uchunguzi kamili wa chanzo cha tukio hilo unaendelea na baada ya kukamilika wananchi watataarifiwa kuwa nini kinaendelea.

Endelea kufuatilia mtandao huu kujua nini kinaendelea wilayani Ludewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa