Na Bertha Lumala
Yanga
SC noma sana! Inachokisema TFF wanafuata na kutekeleza. Ndivyo
unacyoweza kusema. Ulikumbuka tamko la jana la Yanga SC kuhusu
kubaguliwa na kukabwa koo kwa mshambuliaji Amisi Tambwe na nyota wa Ruvu
Shooting? Useme nini tena kwa tamko hili la leo la TFF! Tega sikio…Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limemfungia refa Mohamed Teofile kuchezesha
mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu baada ya
“KUSHINDWA KUIMUDU MECHI YA YANGA SS DHIDI YA RUVU SHOOTING.”Mwenyekiti
wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Chama akiwa Mwanza leo jioni
ameuthibitishia mtandao huu juu ya kufungiwa kwa Teofile kuchezesha
mechi msimu huu.“Ni
kweli tumemwondoa kwenye ratiba ya marefa wa msimu huu Mohamed Teofile
kwa sababu hakuimudu mechi ya iliyopita ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting.
Ni mwamuzi huyo tu ambaye tumemchukulia hatua hadi sasa,” amesema
Chama.
Uamuzi
huo umetoka ikiwa ni siku moja tu, tena saa chache baada ya uongozi wa
Yanga SC kutoa tamko la kuishinikiza TFF kuwafungia marefa waliochezesha
mechi na kuanika hadharani ripoti ya kamisaa wa mechi hiyo
iliyomalizika kwa suluhu.
Katika
mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya Yanga
jijini jana mchana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga,
Jerry Muro alitoa masharti manne kwa TFF kuchukua hatua kali dhidi ya
wachezaji wa Ruvu Shooting, kuwafungia marefa na maofisa wa Ruvu
Shooting pamoja na kutowapanga tena waamuzi husika katika mechi
zinazohusisha kikosi cha Yanga.
Leo
TFF imetekeleza agizo moja wapo bila hata kueleza kikao cha Kamati ya
Waamuzi ya shirikisho kimekaa lini na wapi kupitisha kupitia mkanda wa
video ya mechi na ripoti za marefa na kamishina wa mechi kabla ya kutoa
maamuzi hayo.
Marefa
Michael Mkongwa na Yussuph Sekile waliokuwa wasaidizi wa Teofile pamoja
na Kenneth Mapunda aliyekuwa refa wa mezani Jumamosi hawajaadhibiwa na
kamati ya Chama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni