MATUKIO YA UHALIFU NJOMBE YAONGEZEKA KWA 1.65% MWAKA 2015 UKILINGANISHA NA MWAKA 2014.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani .
Na Michael Ngilangwa NJOMBE
Jeshi La Polisi Mkoani Njombe Limetoa Taarifa Ya Uhalifu Wa Makosa Ya Jinai Kwa Mwaka 2013/2014 Kuwa Yameongezaka Kwa Asilimia 1.65 Tofauti Na Mwaka 2013 Ambapo Kulikuwa Na Jumla Ya Matukio Ya Uhalifu Wa Makosa Ya Jinai 1090 Ambapo Kwa Mwaka 2014 Yamekuwa 11,008 Ikiwa na Ongezeko la Matukio 18.
Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Akiwa Katika Ukumbi Wa Polisi Mkoa Wa Njombe Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa SACPFulgence Ngonyani Ameyataja Baadhi Ya Matukio Yaliopungua Na Kuongezeka Kwa Kipindi Cha Mwaka 2013/2014 Kuwa Ni Pamoja Na Matukio Ya Mauaji Ambayo 2013 Yalikuwa 103 Na Mwaka 2014 Yalikuwa 94.
Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Matukio Ya Unyang'anyi Wa Kutumia Silaha Mwaka 2013 Yalikuwa 6 Na Mwaka 2014 Yameripotiwa Matukio Saba,Unyang'anyi Wa Kutumia Nguvu Yalikuwa 64 Mwaka 2013 Na Mwaka 2014 Yalikuwa 29 Huku Upatikanaji Wa Silaha Mwaka 2013 Yakiwa Mawili Na 2014 Yakiongezeka Hadi Kufikia Matukio 5 .
Akitoa Taarifa Ya Makosa Ya Usalama Barabarani Yaliyo tokea Kwa Kipindi Cha Kuanzia Mwaka 2013 Hadi 2014 Amesema Ni Makosa 14401 Yaliyo Ripotiwa Kipindi Cha Mwaka 2013 Na Mwaka 2014 Ni Makosa 20564 Ambapo Ongezeko Lake Ni
Makosa 6163.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni