Katika hali
isiyokuwa ya kawaida diwani wa kata ya Nyugwa katika halmashauri ya wilaya ya
Nyang’hwale mkoani mkoani Donald Kabosolo (CCM) amenusurika kupigwa na wananchi
wenye hasira kali mara baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi Nyugwa
sekondari.
Tukio hilo
la aina yake lililoshangaza na
kusikitisha wananchi wa mjini hapo na viunga vyake lilitokea jana majira ya
jioni baada ya diwani huyo kumchukua mwanafunzi huyo (Jina Tunalihifadhi) wa kidato
cha tatu kwa ajili ya kufanya nae mapenzi kwenye gesti ya diwani huyo iliyopo
mjini Kharumwa.
Mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa diwani
huyo alikuwa kwenye nyumba yake ya kulala wageni hapo majira ya jioni lakini
baada ya muda walimuona mwanafunzi akifika hapo na kuingia ndani kwa muda mrefu
ndipo walipoweka mtego wa kumnasa kwa vile wananchi wanadai kuwa alikuwa
anafanya nae mapenzi kwa muda mrefu.
"Ninashangaa
kumuona
diwani huyo ambaye ni kioo cha jamii anafanya mapenzi na mwanafunzi ,
kama anataka mwanafunzi angeenda vyuoni ambako kule wanasoma
wameolewa na si hapa kwetu tena kwenye kata yake, huyu anatakiwa
achukuliwe
hatua za kisheria’’alisema mwananchi huyo.
Hata hivyo
diwani huyo baada ya kukamatwa na wananchi huku wakitaka kumshushia kipigo,
baadhi ya wasamaria wema waliwataarifu jeshi la polisi ambapo walifika na
kumpeleka kituoni kwa usalama wake kabla ya kuwekewa dhamana.
Alipotafutwa
diwani huyo kwa njia ya simu yake ya kiganjani alisema kuwa anasikitishwa na
mpango ambao huo umesukwa kutokana na mambo mengi aliyoyaibua katika shule hiyo
yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya viongozi wa shule.
"Mwandishi mimi nashangaa kwamba nimekamatwa na mwanafunzi wa kidato cha tatu tena wa shule yangu sijakamatwa
hata kidogo lakini kuna mambo mengi yalikuwa yanafanywa na viongozi wa shule hiyo
kwa kufisadi mambo katika shule hiyo ndio maana wameamua kunisigizia’’ alisema
diwani.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale
Ibrahimu Marwa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa atahakikisha
diwani huyo anachukuliwa hatua mara moja na wale watakao onekana kumtetea na
wao watachukuliwa hatua.
“Ni kweli
diwani amefanya, kitendo hicho si cha kiungwana kabisa kwani amejidhalilisha yeye
mwenye, familia yake na chama chake nitahakikisha anachukuliwa hatua mara moja,”alisema
Marwa
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Kadama Malunde (Owner)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni