Ijumaa, 23 Januari 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA UNGUJA KASKAZINI

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kikobweni jimbo la
Chaani mkoa wa Unguja Kaskazini  akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja  kuhimiza uhai wa Chama Cha Mapinduzi mahali ambapo kimelegalega na kuongeza nguvu mahali ambapo kinatekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UNGUJA KASKAZINI).2Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akielekea kwenye ukubi wa Mkorea mahali ambapo mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Unguja Kaskazini umefanyika.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za kupanda migomba wakati alipokitembelea kikundi cha akina mama cha  Tuko Imara kinachojishughulisha na shughuli za kilimo cha Migomba, Mbogambona na Mananasi katika kijiji cha  Banda Maji4Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai naye akishiriki kupanda migomba wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokitembelea kikundi hicho na kujionea shughuli zao za uzalishaji wa mazao ya kilimo.5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya kilimo cha mananasi kutoka kwa Bi Mayasa Abdallah Juma Mwenyekiti wa kikundi cha Tuko Imara wakati alipokitembelea kikundi hicho.67Baadhi ya wananchi wakiondoka mara baada ya kufanya kazi ya kusafisha barabara hiyo kwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana9Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi wa nyumba ya madaktari katika kijiji cha Kijini Hospitali jimbo la Matemwe10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia mchezo wa sarakasi uliochezwa na vijana  wa Kijini Hospitali wakati alipotembelea ujenzi wa nyumba wa madaktari katika kijiji hicho1819Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Skuli mjini Nungwi20Baadhi ya wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi zao za uanachama wa chama hicho.21Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwaaapisha wanachama wapya wa CCM kwenye uwanja wa Skuli mjini Nungwi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa