Zaidi
ya watu 40 wamenusurika kifo huku mmoja akikatika viungo vya miguu na
wengine kujeruhika vibaya baada ya lori moja lilionekana kuwa ni la
jeshi kugongana uso kwa uso na gari la abiria aina ya COSTA la Ubungo
-Tegeta eneo la Tegeta jijini Dar es salaam.
Tukio hilo limevuta hisia za mamia ya wakazi wa Tegeta huku baadhi ya
mafundi gereji wa Tegeta wakijaribu kutumia vifaa maalumu kukata mabati
ya magari kwa nia ya kunasua baadhi ya majeruhi walionasa ndani ya
COASTA hiyo kusuru abiria walioonekana kunasa katika vyuma vya magari
hayo.Baadhi ya mashuhuda na dereva wa COSTA pamoja na
kuomba eneo la kibaoni kuweka njia ya mzunguko maarufu kama ROUND ABOUT
kwa lengo la kuepusha madereva wanao lazimika kugeuza kwa dharura
katika njia kuu maarufu kama UTAN kutokana na njia hiyo kukosa fursa ya
kugeuza endapo kuna ulazima wa kufanya hivyo.
Pia wamemtupia lawama Dereva wa Lori kama msababisha ajali kwa kukosa hekima ya kuchukua tahadhari kabla ya kufanya hivyo.
Kamanda wa polisi mkoa kipolisi Kinondoni Kamilius Wambura
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kutoa taarifa mara baada
ya uchunguzi kufanyika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni