Mwanamuziki
anaetamba na hits single ya Akadumba Nay wa Mitego amefunguka na kusema
kuwa katika maisha yake ya utafutaji na kuhangaika na sanaa kuna watu
wengi waliamini kuwa anapoteza muda.
Nay
amesema watu hao pia wanadai kuwa bangi ndizo zinampotezana kufanya
muziki ambao waliamini kuwa unaleta chuki au usingeweza kumtoa na
kumtabulisha kama wasanii wengine ambao walitamba kipindi hicho yeye
akitafuta kutoka.
Nay wa
Mitego alisema kuwa katika kuhangaika na muziki ilifika mahali hata
mzazi wake ambaye ni mama yake mzazi alimfukuza nyumbani kwake akiwa
darasa la saba sababu ya muziki ambao leo umeweza kumfungulia njia na
kumpa mafanikio ambayo hata mzazi huenda anayafurahia.
"Wakati
Naanza kila mtu aliniona kama napoteza muda hivi, wengine walisema bangi
ndo zinanipoteza. Ata mama mzazi alinifukuza nyumbani nikiwa darasa la
Saba sababu ya huu Muziki ninao ufanya sasa."
Mbali na
kukatishwa tamaa Ney anadai kuwa hakuweza kukata tamaa sababu alikuwa
anatambua nini anakifanya hivyo alizidi kukomaa na kuona kuwa anafikia
malengo yake ya kufanikiwa kupitia muziki wa Bongo Fleva na kupata
heshima hata kwa watu ambao walikuwa wanaona anapoteza muda.
"Sijawahi
kukata tamaa nikiamini siku moja nitakuja kufanikiwa na wataniheshimu
wote wanaonidharau..Thnx God kwa kunipa moyo wa ujasiri mpaka nilipo
Leo..!! Angalau naheshimika, nackilizwa..Wengi wao leo wanajivunia
Ney-Wamitego"
Mkali
huyo kupitia ukurasa wake wa Instragram amewataka vijana kutokata tamaa
na wazidi kutafuta pesa kwani hata yeye moja ya ndoto yake ni kuona
anaishi maisha ya kitajiri na anaamini yatatimia hivi karibuni.
"Washkaji
zangu eeh!?? Tutafuteni #Hela tuacheni masihara kabisaa.Kiukweli mimi
napenda kuishi maisha mazuri yakitajiri (like a boss) na nina imani
nitaishi ivyo soon, coz nikikumbuka nilikotoka daah..!!! Huwa sometimes
siamini kama ni Mimi (Ahsante Muziki_Media_Mashabiki).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni