Jumapili, 25 Januari 2015

ZAIDI YA TANI 20 ZA DAGAA NYASA ZAZUIWA BANDARI YA KYELA.

Na Ibrahim Yassin,Kyela
 
ZAIDI ya  tani 20 za dagaa nyasa kutoka wilaya ya Ludewa mkoani Njombe zimezuiliwa kwenye bandari ya Itungi iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya zilizokuwa zikisafirishwa kwenda  kuuzwa mikoani kupitia bandari hiyo.


Hatua hiyo ya kuzuiliwa kwa dagaa hizo kumetokana na hatua ya Serikali wilayani Kyela chini ya mkuu wa wilaya Magret Marenga,kufuatia kuzuka hofu kuwa kuna mgodi wa machimbo nchini Malawi kuvujisha maji machafu yanayodaiwa kuwa na sumu hivyo kuwa na hofu ya kupata madhara pindi walapo samaki hizo.


Kufuatia hofu hiyo Serikali mkoani Mbeya ililifunga soko la Samaki wilayani humo pamoja na kuwazuia wavuvi wasivue samaki hadi pale uchunguzi wa mkemia mkuu wa Serikali aliyechukua sampuli ya samaki hizo kwa ajili ya kuzipima na wataruhusu shughuri za uvuvi na uuzwaji wa samaki pindi majibu ya mkemia yatakapo tolewa.


Ikiwa hali hiyo ipo hivyo zaidi ya wavuvi na wafanyabiashara kumi kutoka wilayani Ludewa waliokuwa wakisafirisha dagaa hizo dagaa zao zimezuiliwa katika bandari hiyo hadi pale majibu ya mkemia yatakapotolewa kama zina sumu au laa.


Kufuati Serikali mkoani Mbeya kuzuia zoezi hilo lakini bado agizo hilo linaonekana kupuuzwa baada ya shughuri za uvuvi kuendelea huku wauzaji wa samaki wakitembeza mitaani bila kificho ambapo wafanyabiashara kutoka Ludewa wakizidi kusota Gest wakisubili majibu ya Mkemia mkuu.


Franko Ngoye,Titto Kayombo na Kevin Haule ni miungoni mwa waliozuiliwa kusafirisha dagaa katika Bandari hiyo walisema wao hawana taarifa ya uwepo wa agizo hilo na kuwa katika wilaya yao Tarafa yote ya Mwambao wanatumia maji ya ziwa hilo kwa shughuri zote ikiwemo kunywa toka enzi za mababu zao.


Walisema walipofika na dagaa hizo tarehe 18 mwezi huu katika Bandari hiyo lengo lao ni kusafirisha kwenda mikoani kwa ajili ya kuziuza lakini samaki hizo zilizuiliwa kusafiriswa wakidai kuna hofu ya samaki hizo kuwa na sumu na kuwa hawakuambiwa wasubiri hadi lini.


Walisema hivi sasa wameishiwa pesa za matumizi na za kulipa Gest na kufikia hatua ya kula mlo mmoja kwa siku na kurudishwa vyumba na kulundikana katika chumba kumoja kutokana na ukosefu wa fedha huku hatma yao kutojulikani.


Waliongeza kuwa Serikali wilayani Kyela imekuwa ikiwanyanyasa miaka mingi pindi wasafirishapo samaki kupitia Bandari hiyo kwa kuwatoza pesa nyingi pamoja na kuwa wanakuwa wanalipia katika wilaya yao na kwamba hulipia Shiling 500 hadi 400 kwa boksi lakini wakija kyela wanaambiwa walipie upya.


Akijibu hoja hizo mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alisema ni kweli Serikali imezuiwa kwa muda kuuza samaki pamoja na wavuvi kuendelea kuvua kwa hofu hiyo ya kuwa ziwa nyasa kuwa na sumu hadi pale majibu ya mkemia mkuu wa Serikali atakapo leta majibu baada ya kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.


Aliongeza kuwa wavuvi hao wavute subira hadi juma tatu kesho majibu yatakuwa tayari,na kwamba kama itaonekana dagaa hao wanansumu watafukiwa shimoni na kama itathibitika kutokuwa na sumu wataruhusu shughuri hizo kuendelea.


Kuhusu wavuvi kukaidi agizo hilo kwa kuendelea kuvua huku wafanyabiashara kuuza samaki hao mitaani alisema inatokana na uongozi wa Serikali wilayani humo kutosimamia ipasavyo zoezi hilo.

Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa