Jumamosi, 24 Januari 2015

RAIS ABADILI MAWAZIRI NA MANAIBU WAO



Waziri wa Nishati na Madini mpya, George Simbachawene.
Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe.

Waziri wa Mahusiano na Uratibu, Mary Nagu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Wiliam Lukuvi.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Steven Wassira.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Christopher Chiza.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Steven Masele.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, Angellah Kairuki.
Naibu Waziri Katiba na Sheria,Ummy Mwalimu.
Naibu Waziri Anna Kilango Malecela, Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amebadili mawazini na naibu mawaziri Ikulu leo.
Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao leo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais,  Sifue Ombeni alitaja mawaziri hao wapya ambao wanaapishwa jioni hii na wizara zao kwenye mabano kuwa George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).
Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).
Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini).
https://www.youtube.com/watch?v=B_Dp_grkVLs

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa