Picha na taarifa za uvamizi wa kituo cha Polisi cha Ikwiriri katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani
Majambazi yaliyojihamu kwa silaha yamevamia Kituo cha Polisi cha
Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua askari wawili na kupora silaha
zilizokuwepo kituoni hapo.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, huku askari wanaodaiwa
kupotenza maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na WP Judith
aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku
polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika tukio la uvamizi, kituo cha
polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani.
Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabomu ya machozi na risasi 60 za SMG.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni