Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakielekea viwanja vya Mkutano wa
hadhara kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana,
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana akipandisha bendera ya
Mabalozi wa jimbo la Uzini Unguja baada ya kukabidhi bendera kwa
mabalozi wote wa jimbo hilo zilizotolewa na Mbunge wa Uzini Mhe.
Mohaamed Seif Khatib.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai akisisitiza jambo
kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya
tunduni Wilaya ya Kati Unguja.
Wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa hadhara wakati Katibu Mkuu wa
CCM akihutubia katika viwanja vya Tunduni Wilaya ya Kati Unguja jimbo la
Uzini.
Mbunge wa jimbo la Uzini Unguja Mhe. Mohammed Seif Khatib akizungumza na
Wananchi wa jimbo lake baada ya kupewa nafasi na Katibu Mkuu wa CCM
Ndg. Abdulrahaman Kinana kutowa maelezo ya kukamilisha ahadi kwa
Wananchi wa jimbo lake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana akiwahutubia Wananchi wa
Wilaya ya Kati Unguja baada ya kumaliza ziara yake katika Wilaya hiyo
kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchanguzi ya CCM na kutembelea miradi
ya maendeleo katika Wilaya hiyo.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia katika viwanja vya mkutano wa hadhara katika jimbo la Uzini Unguja
Mmoja wa Kiongozi wa timu za Mpira katika jimbo la Uzini Unguja
akipokea Seti ya Jezi kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrarnan
Omar Kinana.
Viongozi wa timu 38 za Jimbo la Uzini wakiwa na jezi waliokabidhiwa na
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abulrahaman Kinana zilizotolewa na Mbunge wa
Uzini Mhe. Mohammed Seif Khatib.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana akiwa na kadi tano za
Waliokuwa wanachama wa Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi katika
jimbo la Uzini Unguja Zanzibar
Mwanachama mpya kutoka Chama cha CHADEMA Bi Fatma Kassim akizungumza
baada ya kukabidhiwa Kadi ya CCM na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahan
Kinana, akiwa jukwaani akitowa maelezo kwa Wananchi baada ya kukabidhiwa
kadi katika viwanja vya Tunduni Jimbo la Unguja Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Kinana akimkabidhi
Kadi Mwanachama Mpya wa CCM aliyejiunga kutoka Chama upinzani.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi waliojiunga na CCM kutoka vyama vya
Upinzani wakila kiapo cha Utii wa Chama baada ya kukabidhiwa kadi zao na
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulraham Kinana.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahaman Omar Kinana akijumuika na Wanachapa wapya wa CCM waliojiunga na CCM na jumuiya za Chama hicho, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Tunduni jimbo la Uzini Unguja Zanziba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni