Na Ibrahim
Yassin,Kyela
ZAIDI
ya tani 20 za dagaa nyasa kutoka wilaya
ya Ludewa mkoani Njombe zimezuiliwa kwenye bandari ya Itungi iliyopo wilayani
Kyela mkoani Mbeya zilizokuwa zikisafirishwa kwenda kuuzwa mikoani kupitia bandari hiyo.
Hatua hiyo
ya kuzuiliwa kwa dagaa hizo kumetokana na hatua ya Serikali wilayani Kyela
chini ya mkuu wa wilaya Magret Marenga,kufuatia kuzuka hofu kuwa kuna mgodi wa
machimbo nchini Malawi kuvujisha maji machafu yanayodaiwa kuwa na sumu hivyo
kuwa na hofu ya kupata madhara pindi walapo samaki hizo.
Kufuatia
hofu hiyo Serikali mkoani Mbeya ililifunga soko la Samaki wilayani humo pamoja
na kuwazuia wavuvi wasivue samaki hadi pale uchunguzi wa mkemia mkuu wa
Serikali aliyechukua sampuli ya samaki hizo kwa ajili ya kuzipima na wataruhusu
shughuri za uvuvi na uuzwaji wa samaki pindi majibu ya mkemia yatakapo tolewa.
Ikiwa hali
hiyo ipo hivyo zaidi ya wavuvi na wafanyabiashara kumi kutoka wilayani Ludewa
waliokuwa wakisafirisha dagaa hizo dagaa zao zimezuiliwa katika bandari hiyo
hadi pale majibu ya mkemia yatakapotolewa kama zina sumu au laa.
Kufuati
Serikali mkoani Mbeya kuzuia zoezi hilo lakini bado agizo hilo linaonekana
kupuuzwa baada ya shughuri za uvuvi kuendelea huku wauzaji wa samaki
wakitembeza mitaani bila kificho ambapo wafanyabiashara kutoka Ludewa wakizidi
kusota Gest wakisubili majibu ya Mkemia mkuu.