Jumapili, 31 Mei 2015
January Makamba: Taifa liko njia panda, Wananchi Chagueni Kiongozi Atakayeleta Maendeleo
NAIBU
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, amesema
kwa sasa nchi ipo njia panda, hivyo kuna haja ya kutumia busara ili
kuchagua kiongozi atakayeleta maendeleo.
CHADEMA Wamteua Godbless Lema kuwa Kamanda wa Operesheni ya Uandikishaji wa Daftari la Wapigakura
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kaskazini, kimemchagua
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Godbless Lema, kama Kamanda wa
Operesheni ya Uandikishaji wa Daftari la Wapigakura katika kanda hiyo.
NDIVYO ILIVYOKUWA JANA NDANI YA JIJI LA ARUSHA KATIKA MKUTANO WA LOWASA.....................
Mtangaza
nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono
maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza
nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono
maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MAAJABU:ONA MWANAUME ALIVYOPANDIKIZIWA USO WA MTU MWINGINE BAADA YA USO WAKE KUARIBIKA NA KUWEKEWA SURA YA MTU ALIYEKUFA
Picha ikimwonyesha Norris kabla hajapata ajali, alivyopata ajali na baada ya kuwekewa uso mwingine wa marehemu |
Ajali nyingi duniani zimekua
zikisababisha vifo vya watu wengi huku zikiacha wengine wakiwa na
ulemavu wa maisha ambao huwasababishia kupoteza mwelekeo wa maisha yao
na kukata tamaa kabisa.
Jumamosi, 30 Mei 2015
MOI Yaongoza kwa Upasuaji Kidunia
TAASISI
ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imetangazwa kitovu cha weledi
duniani katika upasuaji wa mfupa mrefu wa paja na wa chini ya goti
kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wenye
mafanikio makubwa kuliko nchi nyingine yeyote duniani.
Wema Sepetu na Idris Nusura Wazichape
Malkia anayemiliki Kampuni ya Endless Fame
Production, Wema Isaac Sepetu na Mshindi wa Big Brother Africa 2014/15,
Idris Sultan ambao wamekuwa marafiki wakubwa katika siku za hivi
karibuni, nusu wazichape kavukavu baada ya kupishana kauli huku wivu wa
kimapenzi ukitajwa.
Ijumaa, 29 Mei 2015
Kina Mramba na Daniel Yona Kuhukumiwa Juni 30......Wanakabiliwa na Matumizi Mabaya ya Ofisi
Lowassa aitikisa Arusha......Watu wafurika, Wakosa vyumba Walala katika Magari, wengine wajiapiza Kulala Uwanjani....... Mkuu wa Majeshi mstaafu naye Atinga, fulana zenye Picha yake Zapanda Bei
NYUMBA
za kulala wageni katika Jiji la Arusha na viunga vyake zimeanza
kufurika kutokana na makundi ya watu yanayowasili jijini hapa kushuhudia
mwanzo wa ‘Safari ya Matumaini’ ya Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa
Monduli Edward Lowasa, anayoianza rasmi leo.
Jumatano, 27 Mei 2015
TANZANIA KUTOA NAFASI ZAIDI KUWEZESHA WAKIMBIZI KUWA NA MAISHA YA KAWAIDA DSC_0009
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa ndege Kigoma akiwa
ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo
pichani) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia) na kupokelewa na
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo,
Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto) kwa ajili ya kutembelea na
kuona changamoto katika maeneo maalum wanapohifadhiwa Wakimbizi. Kulia
ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma
Abdulla Saadala.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
KALI YA MWAKA :SPIKA ANNA MAKINDA "AISIFIA" BANGI YA NJOMBE BUNGENI
Spika wa Bunge Anne Makinda amesema
bangi inayolimwa katika Mkoa wa Njombe si kali kama inayolimwa Mikoa
mingine kutokana na baridi kali iliyopo Mkoani humo.
NYERERE APEWA TUZO
ALI KIBA NA JOKATE Penzi ni Kikohozi Uwezi Kulificha, Wathibitisha Uhusiano wao kwa Picha Hizi
RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN AFUNGA MKUTANO WA MABALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JIJINI DAR
Balozi
Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dr. Ali Mohammed Shein akiufunga Mkutano wa Nne wa siku Tatu wa
Mabalozi wa Tanzania uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Ramada Mjini
Dar es Salaam.
Wizi TTCL Unatisha......Kambi Ya Upinzani Yaibua Tuhuma Nzito, Serikali Yabanwa Itoe Majibu
KAMBI
Rasmi ya Upinzani bungeni, jana imeibua tuhuma nzito bungeni Mjini
Dodoma dhidi ya Kampuni ya Simu nchini (TTCL), ikidai aliyekuwa Meneja
Biashara wa kampuni hiyo (bila kutajwa jina), amefungua akaunti nchini
yenye kiasi cha sh. bilioni moja.
Jumanne, 26 Mei 2015
BVR Kigoma yalalamikiwa......Wananchi Walala Kituoni Kujiandikisha
Zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa
kielektoronik BVR umelalamikiwa na wananchi katika manispaa ya Kigoma
Ujiji kutokana na kuchelewa kuandikishwa licha ya wananchi kulala kwa
zaidi ya siku mbili katika vituo vya kuandikishia.
K-Lynn azungumzia maisha yake kama mama, kwanini hawezi kurudi kwenye muziki na kazi ya interior design
Ni nadra sana kukutana na Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi maarufu kama
K-Lynn lakini kupitia tuzo za watu tulifanikiwa kupiga story mbili tatu.
Filamu ya Van Vicker na Wema Sepetu ‘Day After Death’ kuzinduliwa September, Dar
Filamu ya Wema Sepetu na muigizaji wa Ghana, Van Vicker ‘Day After
Death’ inatarajiwa kuzinduliwa September mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Jumamosi, 23 Mei 2015
Unajua Wema Sepetu Kazaliwa lini? Na Johari Je?......Unataka kujua Wanatoza Shilingi Ngapi Kucheza Muvi Moja?? Bofya hapa
Kila mwanamichezo au mwanamuziki hulipwa mshahara
kulingana na kiwango chake, hali hii ipo hivyo pia kwa waigizaji na watu
wengine wa kawaida.
Jumatano, 20 Mei 2015
Wanafunzi wa chuo kikuu cha UDSM wagoma kuingia darasani kwa madai ya kutopewa fedha za kujikimu.
Kipindupindu Chalipuka kwa wakimbizi wa Burundi Walioko Katika Kambi ya Kigoma.
WAKATI
hali ya usalama nchini Burundi ikiwa bado tete, wakimbizi 558 walioko
katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma wanaugua ugonjwa wa
Kipindupindu.
Jumatatu, 11 Mei 2015
Wanafunzi 'WAPIGWA' Mkutano Ukawa Arusha
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wanafunzi wa shule za msingi za Mwangaza na Ngarenaro, juzi walidaiwa kupata kipigo kutoka kwa vijana waliojiita ‘Makamanda’ wa umoja wa vyama vya siasa vya upinzani ujulikanao kama Ukawa, baada ya baadhi yao kufika katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya karibu na shule yao.
Jumapili, 10 Mei 2015
Pinda: Tumedhamiria kuitokomeza malaria
WAZIRI
Mkuu, Mizengo Pinda, amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la
ugonjwa wa malaria kwa kuamua kujenga kiwanda cha kisasa cha kutengeneza
dawa za kuua viluwiluwi wa mbu wanaosababisha ugonjwa huo.
Maandamano Burundi yachukua sura mpya
Serikali ya Burundi imewataka waandamanaji katika mji mkuu wa
Burundi Bujumbura kusitisha maandamano yao dhidi ya hatua ya rais wa
taifa hilo Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa
mwezi ujao.
Kenya wamtaka Rais Kikwete kuingilia kati mgogoro Burundi
Wananchi nchini Kenya wamemtaka mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambaye ni Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete kuingilia kati
mgogoro wa Burundi uliopelekea wanachi zaidi ya kumi kufariki dunia na wengine
kukimbilia nchini Tanzania.
Diwani CUF Mbaroni kwa Tuhuma za Kuomba na Kupokea Rushwa ya Sh 150,000
FILIKUNJOMBE AWEKA HISTORIA LUDEWA
Filikunjombe akikabidhi kitanda cha kujifungulia katika kijiji cha Mavanga
Jumamosi, 9 Mei 2015
Mgawanyo Wa Majimbo UKAWA: CHADEMA Yaachiwa Jimbo Moja Zanzibar
UMOJA
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umeridhia Chama cha Wananchi (CUF)
kusimamisha wagombea wake wa nafasi ya ubunge katika majimbo yote ya
uchaguzi visiwani Zanzibar, isipokuwa katika Jimbo la Kikwajuni.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Makao Makuu ya CUF, Mkurugenzi wa
Oganaizesheni na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Sheikh, alisema Ukawa
wamekubaliana katika Jimbo la Kikwajuni watasimamisha mgombea ubunge
kutoka Chadema ambaye ni Salum Mwalimu.
Mwalimu ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), ambaye hata hivyo tangu ateuliwe amekuwa akifanya kazi zake Tanzania Bara.
Jimbo
la Kikwajuni linaunganisha wakazi wa maeneo ya Kikwajuni Juu na Chini,
Kisimamajongoo, Kilimani, Miembeni, Magereza na sehemu ya eneo la
Michenzani.
Uamuzi
wa Mwalimu kusimama kuwania ubunge Jimbo la Kikwajuni kupitia Chadema,
umepokewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wachambuzi wa siasa ndani ya
jimbo hilo huku wakionesha uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 30
huenda utaleta changamoto kubwa kwa CCM.
Changamoto
kubwa inayoonekana kwa CCM ni kwamba, Mwalimu amezaliwa na anatoka
katika familia yenye makazi katika eneo maarufu la Kisimamajongoo ambalo
lilikuwa ni kitovu cha harakati za siasa za Chama cha Afro Shiraz
(ASP).
Wachambuzi
wanasema kwa namna moja ama nyingine familia ya Mwalimu nayo ilishiriki
kinagaubaga katika harakati za kudai ukombozi kwa Mzanzibari
zilizofanywa na hayati Mzee Karume.
Eneo
la Kisimamajongoo ndilo lilikuwa kitovu cha harakati za ASP kudai uhuru
wa Mzanzibari kutoka kwa Sultani na Wanamapinduzi walikuwa wakikutana
katika eneo hilo kupanga mikakati yao wakiongozwa na hayati Mzee Karume
katika nyumba yake aliyoipa jina la ‘Ndiyo’.
Hata hivyo, zilipokuja siasa za ushindani, baadhi ya wakazi wake wakagawanyika na kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF).
Wakazi
wa eneo la Kisimamajongoo wanaaminika ni ndugu wa damu na hilo ndilo
linasemwa huenda likawa ni moja ya jambo litakalowavutia wananchi wa
jimbo hilo kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuamua kumpa uongozi
Mwalimu wakiamini ni kijana wao na hatowaangusha.
Mwalimu
licha ya kuwa amezaliwa katika eneo la Kisimamajongoo, lakini
wachambuzi wanasema pia katika uchaguzi huo atabebwa sana na umaarufu wa
mama yake mzazi ambaye ni mtangazaji maarufu nchini, Faudhiyat Ismail
Aboud.
Kwa
sasa Jimbo la Kikwajuni kwa nafasi ya ubunge linaongozwa na Hamad
Yussuf Massauni (CCM), ambaye pia ni mzaliwa wa eneo la Kisimamajongoo
na hata katika uchaguzi wa mwaka 2010 alibebwa na turufu hiyo.
Inaaminika
katika uchaguzi huo wananchi wote wa Jimbo la Kikwajuni kwa pamoja
wakiongozwa na kampeni zilizofanywa na wakazi wa eneo la Kisimamajongoo,
waliamua kumpa kura Hamad wakiamini kuwa ni kijana wao.
Wachambuzi
wanasema uamuzi wa Ukawa kumsimamisha Salum Mwalimu, umefanywa
kiutafiti zaidi wakiamini utaamsha ushindani mkubwa katika jimbo hilo
ambalo limekuwa chini ya mikono ya CCM miaka yote.
Katika
hatua nyingine, Mbunge wa Mji Mkongwe, Ibrahim Sanya, anatarajiwa
kusimama tena kutetea nafasi yake katika uchaguzi ujao akichuana na
Mwanahabari Maarufu, Ally Saleh ambaye ameshatangaza nia.
Katika nafasi ya Uwakilishi, CUF imemteua Ismail Jussa Ladhu kuwania nafasi hiyo akiwa ndiye mgombea pekee kutoka chama hicho.
Wakati
huo huo, Mwandishi wetu kutoka Zanzibar, Is-haka Omar, anaripoti kuwa,
CUF Zanzibar kimeeleza kuwa hatua yake ya kuendelea na mchakato wa
uchaguzi ndani ya chama hicho katika majimbo 49 ya Zanzibar haiendi
kinyume na makubaliano ya umoja huo.
Chama
hicho kimesema hatua hiyo haitaathiri makubaliano kati ya vyama hivyo
ya kuachiana majimbo katika uchaguzi mkuu ujao baada ya umoja huo
kuridhia chama hicho kusimamisha wagombea katika nafasi zote za
uchaguzi.
Pia
CUF imesema jumla ya wanachama 327 wa chama hicho wamepitishwa kuomba
kuteuliwa kugombea nafasi za ubunge na uwakilishi wa majimbo na katika
viti maalumu vya wanawake Zanzibar.
Kati
ya wanachama hao, 133 wameteuliwa kugombea ubunge, 134 uwakilishi
katika majimbo 49 huku wengine 29 wameteuliwa kugombea ubunge kupitia
viti maalumu sawa na wengine 30 walioteuliwa kugombea uwakilishi.
Wagombea
hao watapigiwa kura na wajumbe wa mikutano mikuu ya majimbo na wilaya
ili kupatikana kwa mgombea mmoja ambaye ataidhinishwa na kikao cha
baraza kuu la chama hicho.
Katika
hatua nyingine chama hicho kimeendelea kusisitiza kuitaka ofisi ya
vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi kuwapatia wananchi vitambulisho hivyo
kabla ya kuanza kwa uandikishaji wa duru la mwisho unaotarajiwa kuanza
wiki ijayo katika Jimbo la Micheweni ili kuepuka vurugu.
Bilioni 8 Kutumika Kupanga Upya Jiji la Mwanza
SERIKALI
inakusudia kutumia Sh bilioni nane katika mpango wake wa kulipanga upya
Jiji la Mwanza kwa kuainisha sehemu za makazi, viwanda, biashara na
huduma za kijamii.
Jumatano, 6 Mei 2015
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)