Jumanne, 26 Mei 2015

Filamu ya Van Vicker na Wema Sepetu ‘Day After Death’ kuzinduliwa September, Dar


Filamu ya Wema Sepetu na muigizaji wa Ghana, Van Vicker ‘Day After Death’ inatarajiwa kuzinduliwa September mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wema ameiambia Mpekuzi kuwa Van Vicker atakaa kwa wiki mbili zaidi kwaajili ya kufanya filamu nyingi na muigizaji huyo  aliyeibuka na tuzo ya muigizaji wa kike anayependwa kwenye tuzo za watu zilizotolewa Ijumaa iliyopita.
 
“Tunaplan kuilaunch movie yetu mwezi wa tisa, kaniambia kwamba akija he is going to stay for another two weeks na anategemea tutafanya shoot nyingine huku huku,” amesema Wema.
 
Wema amedai amefurahia kufanya kazi na Van Vicker ambaye jana alimpongeza kwa ushindi wake wa tuzo za watu.
 
“Congrats @wemasepetu on your award for ‘Best & Loved’ Actress 2015. You deserve it. #DayAfterDeath our movie together should take you another notch higher. Thanks for trusting me. #HatsOff4U #TheYoungGodFather #TheEntrepreneur #TheVanVickerBrand,” aliandika Van kwenye Instagram.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa