Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa ndege Kigoma akiwa
ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo
pichani) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia) na kupokelewa na
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo,
Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto) kwa ajili ya kutembelea na
kuona changamoto katika maeneo maalum wanapohifadhiwa Wakimbizi. Kulia
ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma
Abdulla Saadala.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team, Kigoma
Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe
amesema Tanzania itatoa nafasi zaidi kuliko ya sasa ili kuweza kuwaweka
wakimbizi wa Burundi wanaoingia nchini katika mazingira ya kuishi maisha
ya kawaida.Kauli hiyo ameitoa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma jana
kabla ya kuelekea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na kujionea hali
ilivyo akiambatana na watendaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
yaliyopo nchini.
Alisema kama taifa wameona uwingi wa
Wakimbizi na watatoa nafasi zaidi ili kuwezesha Wakimbizi hao kupata
mahitaji yao ya msingi kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa kuhusu
Wakimbizi. Alisema katika kufanikisha suala la kuhudumia Wakimbizi
wanaomiminika kwa sasa serikali itashirikiana na Mashirika ya Umoja wa
Mataifa kuhakikisha mahitaji ya msingi kwa Wakimnbizi hao yanapatikana.
“Wakimbizi wanahaki ya kulindwa na
kuthaminiwa kama wananchi wa Tanzania, kwa hiyo serikali itatoa nafasi
zaidi na tunashukuru msaada tunaopata kutoka kwa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa kukabiliana na tatizo hili …,” alisema.Naye Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja wa Mataifa unatiwa shaka
na hali ya kisiasa ilivyo nchini Burundi na kusema kuyumba kwa hali ya
kisiasa kunaweza kuleta Wakimbizi wengi nchini.
Alisema kwa sasa Umoja wa Mataifa
unafanya kazi na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika na
wanachama wengine wa jumuiya za kimataifa kuhakikisha kwamba hali ya
usalama inarejea nchini Burundi. Aidha aliipongeza Tanzania kwa kuwa
mstari wa mbele kusaidia kutatuliwa kwa mgogoro wa Burundi.
Rodriguez alisema Tanzania ni mfano wa
kuigwa kwa namna inavyoshughulikia Wakimbizi na kusema Umoja wa Mataifa
unaangalia hali inayojitokeza Burundi kwa makini ili kusaidia Tanzania
isilemewe na Wakimbizi. Aidha alisema kwamba kitendo cha serikali ya
Tanzania kutoa nafasi zaidi ya kuwezesha kusiwepo na msongamano wa
Wakimbizi Nyarugusu kunaonesha ushirika wa kweli kati ya serikali ya
Tanzania na jumuiya ya Kimataifa katika kushughulikia matatizo ya
Wakimbizi.
Alisema hata hivyo kuanzishwa kwa kambi
hiyo mpya ni gharama kubwa na kuitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia
kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya. Aidha alisema kwamba Mashirika ya Umoja
wa Mataifa yakifanyakazi kama shirika moja, chini ya uongozi wa Shirika
la Umoja wa mataifa la kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) wameitikia
wanavyostahili pamoja na changamoto nyingi walizokumbana nazo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe akisamiana na Waziri wa Kamanda wa Jeshi la Polisi
mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui (kulia) pamoja na
viongozi wengine wa usalama wa mkoa wa Kigoma mara tu baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma akiwa na mwenyeji wake Kaimu Mkuu
wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi
Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto).
Changamnoto hizo ni pamoja na uwingi wa
Wakimbizi waliokuwa wakimiminika, umbali uliopo wa kambi ya Kagunga
ambako walikuwa wanafikia huku waliowengi wakiwa wanawake na watoto.
Alisema hata hivyo UNHCR walifanikiwa
kuwasajili Wakimbizi hao na kuandaa mazingira ya ukazi wao katika kambi
ya Nyarugusu. Aidha wamewezesha usafiri kwa Wakimbizi kutoka Kagunga
hadi Kigoma. Pia alisema IOM walifungua njia kutoka Kagunga hadi eneo
jirani ambako Wakimbizi walipakia katika mabasi na kufika katika vituo
walivyotakiwa kuwepo.
Pia UNICEF waliweza kusaidia maji na
vifaa vya usafi kwa watoto na WFP wao walihakikisha chakula kinafikishwa
hasa biskuti za kuongeza nguvu.
Aidha WHO wao walikuwa wanaisaidia
serikali katika kukabiliana na mlipuko wa Kipindupindu. Aidha UNFPA
walishughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Mratibu huyo alisema kwamba hata hivyo mambo yote hayo yasingefanikiwa
kama si kwa msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
Mratibu huyo alisema kuwa Mashriika ya
Umoja wa Mataifa yameanza kupata fedha za kusaidia katika shughuli zao
na kwamba kuna ahadi ya dola za Marekani milioni 12.
Alisema kwamba Umoja wa Mataifa umeona
kwamba kutitirika kwa Wakimbizi hao kumeleta hali ngumu kwa serikali ya
Tanzania na wakazi wa Kigoma.Alisema wanatambua changamoto
zinazoambatana na kuwa na kundi kubwa la Wakimbizi lakini wataendelea
kuhitaji msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika
kipindi hiki kigumu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe akiendelea kusamiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa
Kigoma waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina
mwandamizi, Ferdinand Mtui mara tu baada ya kuwasili akiwa amefuatana na
Waziri Chikawe (hayupo pichani).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe (kulia) akifurahi jambo na Mkuu wa ofisi ya Shirika la
Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah
Assiama-Hillgartner kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma mara tu baada ya
kuwasili.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji
(I.O.M), Bw. Damien Thuriaux (kulia) mara tu baada ya kuwasili mjini
Kigoma tayari kuelekea kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akifafanua jambo
kwa viongozi wenzake mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege
mjini Kigoma. Wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez,
Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la
Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(kushoto) akiongozana na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji
(I.O.M), Bw. Damien Thuriaux kuelekea chumba maalum cha mapumziko mara
tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye chumba maalum cha wageni
mashuhuri katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma. Kushoto ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akimsikiliza Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole (katikati) walipokuwa kwenye chumba cha mapumziko.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini
kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kabla ya kusomewa
kwa taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi mkoani Kigoma.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia
ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru akisoma
taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mh. Mathias Chikawe aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la
Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole katika ukumbi wa mikutano
wa ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini Kigoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe akizungumza kwenye mkutano wa kupokea taarifa fupi ya
hali ya wakimbizi katika mji wa Kigoma na changamoto wanazokabiliana
nazo mbele ya wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa
nchini.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akizungumzia jitihada zilizofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika
lake la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi katika
kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa haraka zaidi ili
wakimbizi nao wafarijike kama binadamu wengine
sambamba na sheria za Umoja wa Mataifa zinavyotaka. Kushoto ni Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na watatu kulia ni
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),
Joyce Mends-Cole.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akiendelea na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa ulinzi na usalama wa
mkoa wa Kigoma.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole akizungumza
katika mkutano huo ambapo ameipongeza serikali ya Tanzania kwa moyo wake
wa upendo na kutenga maeneo maalum ya kuhifadhi Wakimbizi kutoka nchi
za jirani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.
Mathias Chikawe katika picha ya pamoja ya viongozi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa na wa mkoa wa Kigoma sambamba wafanyakazi wa Mashirika
mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yaliyopiga kambi mkoani Kigoma kuhudumia
Wakimbizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni