TAASISI
ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imetangazwa kitovu cha weledi
duniani katika upasuaji wa mfupa mrefu wa paja na wa chini ya goti
kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wenye
mafanikio makubwa kuliko nchi nyingine yeyote duniani.
Akizungumza
na Mpekuzi jana jijini Dar es Salaam Meneja Ustawi na Uhusiano wa
Taasisi hiyo Almas Jumaa, alisema zaidi ya Zaidi ya wagonjwa 4800
wamefanyiwa upasuaji wa mifupa mirefu toka Mwaka 2008.
Alisema
katika mwaka huo Taasisi ya MOI ilianza kutumia utaalamu wa kutibu
mifupa iliyovunjika kwa kuweka vyuma maalum vinavyojulikana kama ‘SIGN
NAIL’ tiba ambayo inamfanya mgonjwa aweze kupona kwa haraka na aweze
kurudi katika hali yake ya kawaida.
Alisema
kutokana na mafanikio hayo ya kutibu wagonjwa wengi na kwa weledi nchi
nyingine duniani zimekuwa zikija kwenye taasisi hiyo kujifunza.
“Juzi
tulimaliza mafunzo ya siku tatu ambayo yalikutanisha wataalamu wa
upasuaji kutoka nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kujifunza namna ya
kutibu mifupa mirefu na mingine kama kiunoni na chini ya goti kwa
kutumia teknolojia ya kuweka vyuma,” Alisema Jumaa.
Allizitaja
nchi zilizohudhuria mafunzo hayo kuwa ni pamoja na Nigeria, Zimbabwe,
Ethiopia, South Sudan, Liberia, Haiti na Marekani.
Alibainisha
kuwa, madaktari bingwa kutoka Marekani waliwafundisha mbinu ya
kufidia kipande cha mfupa kilichopotea baada ya ajali kwa kuweka mfupa
wa bandia na kuunganisha mfupa hivyo kumuondoa mgonjwa katika hatari ya
kupoteza kiungo kurudi katika hali ya kawaida.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni