Filikunjombe akikabidhi kitanda cha kujifungulia katika kijiji cha Mavanga
Filikunjombe akikabidhi saruji na Bati kwa walimu wa shule ya msingi Mfaranyaki Mavanga
Filikunjombe akikabidhi saruji na bati kwa viongozi wa kanisa la Anglikan Lupanga
Filikunjombe akiwapungia mikono wananchi wa mavanga wakati akiwasili kijijini hapo
Filikunjombe akiongea na wananchi wa Lupanga
Wananchi wa Mavanga walivyompokea Filikunjombe kwa shangwe
Filikunjombe akipiga mndele kijiji cha Mavanga
Wananchi wa Lupanga wakiwa na furaha kwa kumpokea mbunge wao
Filikunjombe akicheza na watoto wa chekechea ya Mundindi
Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monica Mchilo akiongea na wananchi wa Mavanga katika mkutano wa hadhara
Hizi ni moja ya zawadi anazopewa na wananchi wake anapowatembelea vijijini
Hizi ni moja ya zawadi anazopewa na wananchi wake anapowatembelea vijijini
Mbunge wa
jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh.Deo Filikunjombe amekuwa ni mbunge wa
kwanza katika wilaya ya Ludewa tokea Tanzania kupata uhuru kwa kutimiza ahadi
zake kwa wakati ikiwa ni historia ya kwanza kwa wananchi ambao kwa miaka mingi
wamekuwa na kiu ya maendeleo bila mafanikio.
Hayo
yametokea jana katika kata ya Mavanga na Lupanga ambako Mh.Filikunjombe alikuwa
akikamirisha kutoa ahadi zake katika sekta mbalimbali lakini kubwa zaidi ni
lile la kutoa vitanda vya kujifungulia na darubini ya kupima mgonjwa mbalimbali
ikiwa ni siku ya akina mama Duniani ambapo aliazimisha katika kata hizo kwa
kutimiza ahadi zake za vitanda hivyo viwili vya kujifungulia akina mama.
Akihutubia
katika mkutano wa hadhara uliofantyika katika nyakati tofauti katika kata hizo
wilayani hapa Mh.Filikunjombe alisema kuwa kutokana na umuhimu wa akina mama
Duniani imempasa kununua vitanda hivyo viwili ambavyo vimegharimu kiasi cha
shilingi milioni 5 kwani wanasiasa walio wengi wamekuwa wakiwasahau watu hao
muhimu ambao ndiyo nguzo ya taifa.
Alisema
katika nafasi yake ya ubunge amekuwa ni mbunge wa kuwatumikia wananchi waliompa
ridhaa ya kuwaongoza hivyo amekuwa akitumia kiasi cha fedha yake anayolipwa
Mbungeni kwa kuwarudishia wananchi katika manunuzi ya vifaa kama
Darubini,vitanda na vinginevyo kwani wananchi wa wilaya ya Ludewa ndiyo wenye
mamlaka na pesa yake.
‘’sijaanza
leo kuyafanya haya ninayoyafanya kwani tokea sijawa mbunge na hata nilipopata
ubunge nimeendelea kushirikiana na wananchi wa wilaya yangu katika kuleta
maendeleo ili kuibadirisha wilaya yetu hivyo ninachowaomba wananchi ni
kuvitunza vifaa hivi ili viweze kutumika katika kizazi kilichopo na kijacho’’,alisema
Mh.Filikunjombe.
Vitu vingine
alivyovitoa kwa wananchi ni pamoja na bati 300 mita 3 geji 28 kanisa la
Anglikan Mavanga bati 50 na saruji mifuko 50 shule ya msingi Mfaranyaki kata ya
Mavanga,rangi ndoo 20 na saruji mifuko 50 shule ya Sekondari ya kata ya Mavanga
bati 25,saruji mifuko 25 katika shule ya chekechea mavanga,bati miamoja katika
ujenzi wa kituo cha maenndeleo kanisa katoliki mavanga.
Vingine ni
bati sabini katika kanisa katoliki la kinyika kata ya Lupanga,Bati miamoja
kanisa la Anglikan Lupanga, saruji miamoja na bati miamoja katika shule ya
msingi Lupanga kitu ambacho kimevunja rekodi ya wabunge wote waliowahi
kuiongoza wilaya ya Ludewa na kufikia kukamilisha ahadi alizozitoa kwa wananchi
wa jimbo la Ludewa.
Aidha diwani
wa kata ya Ludewa mjini Mh.Monica Mchilo aliwataka wananchi wa kata hizo kuunga
mkono juhudi za Filikunjombe kwani yote anayoyafanya yapo katika ilani ya chama
cha mapinduzi hivyo anatekeleza ilani ya CCM hivyo kina mmoja atafakari yale
mazuri ya chama ambayo ni msingi wa maendeleo katika wilaya ya Ludewa.
Mh.Mchilo
alikili kuwa ahadi za mbunge huyo zimetekelezeka kwa muda muafaka hivyo hiyo ni
historia mpya wilayani Ludewa kwani hakuna mbunge ambaye aliwahi kuyafanya haya
ambayo yanafanywa na Filikunjombe katika suala zima la uletaji wa maendeleo
wilayani Hapa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni