Siku mbili baada makada waliokuwa wamefungiwa kwa makosa ya kukiuka kanuni za CCM kuachiwa huru, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameeleza nia yake kuwa wakati ukifika atachukua fomu kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Membe alibainisha nia hiyo kwa mara ya kwanza juzi
usiku wakati akihojiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) na kuwa
atatangaza azma hiyo muda wowote kuanzia sasa akiwa jimboni kwake,
Mtama mkoani Lindi.
“Sasa ni rasmi kuwa nina nia ya kugombea urais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Nitatangaza nikiwa kijijini kwangu…
mahali nilipoanzia safari ya kwenda shule, safari ya kwenda usalama wa
Taifa na safari ya kwenda Wizara ya Mambo ya Nje,” alisema.
Membe alikuwa miongoni mwa makada sita CCM
waliokuwa wamefungiwa kwa takriban miezi 17 kwa makosa ya kukiuka kanuni
za uchaguzi wakituhumiwa kuanza kampeni mapema kinyume na taratibu za
chama hicho kilicholazimika kuwachukulia hatua za kinidhamu.
Makada hao walifungiwa tangu Februari, 2014 na
pamoja naye ni mawaziri wakuu wa zamani; Frederick Sumaye na Edward
Lowassa; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira; Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge
wa Sengerema, William Ngeleja.
Akifafanua juu ya dalili za kutimia kwa ndoto yake
za kuiongoza nchi, Membe alisema Mwenyezi Mungu ana namna nyingi za
kufikisha ujumbe kwa mja ampendaye katika kumtumikia kwa mtindo autakao
yeye.
“Nimegundua kuwa unaposema naomba nioteshwe… naomba nioteshwe kumbe Mungu anayo namna nyingine. Anawaotesha wengine kwa ajili yako na ndivyo alivyofanya,” alisema.
“Nimegundua kuwa unaposema naomba nioteshwe… naomba nioteshwe kumbe Mungu anayo namna nyingine. Anawaotesha wengine kwa ajili yako na ndivyo alivyofanya,” alisema.
Kuhusu hilo, Membe alisema kila mtu anasubiri
kuona CCM inatoka vipi na hata vyama vya upinzani vinasubiri hilo na
ndiyo maana navyo vimenyamaza.
Mpaka sasa ni chama cha Tanzania Labour (TLP), kilichokwisha teua mgombea wake wa urais katika uchaguzi huo, Macmillan Lyimo.
“Watanzania wote macho yao yapo CCM, wanasubiri
kuona inafanya nini. Tunaona vyama vingine vimekaa kimya, wanasubiri
CCM iseme ili nao wafuate. Wanapiga kelele za Ukawa…Ukawa lakini
hawawezi kufanya chochote. Hata kama tutasogeza muda mbele bado
wataendelea kusubiri,” aliongeza.
Hali ya usalama Burundi
Waziri huyo pia alitumia nafasi hiyo kuzungumzia
hali ya usalama inayoendelea kuyumba nchini Burundi kwamba kikao cha
mawaziri kinatarajia kuketi baada ya muda mfupi jijini Arusha ili kuona
namna ya kutatua mzozo uliopo.
Alisema Tanzania isingekwa radhi kuona mapinduzi
ya utawala wa Rais Pierre Nkuruzinza yanafanywa wakati akiwa nchini tena
kwa mwaliko na gharama za nchi hii. Alisema hiyo ingemaanisha Tanzania
inahusika nayo.
“Hilo haliwezi kufanyika kwa nchi hii. Tulilazimika kumrudisha
na kama wanataka kufanya mapinduzi wayafanye wote wakiwa huko. Tanzania
siyo nchi ya kuichezea na tusingeweza kukubali kuona hilo linatokea."
Alitanabaisha utata uliojitokeza baada ya Rais
Nkuruzinza kutaka kugombea tena muhula wa tatu kuwa ulishafafanuliwa na
mahakama nchini humo ambayo ilimruhusu kugombea.
“Tuliposuluhisha mgogoro wao wa awali, Bunge lao
la mpito liliridhia kuwa Nkurunziza aiongoze nchi hiyo mpaka uchaguzi
mkuu utakapofanyika.
"Aliiongoza Burundi kwa miaka mitano uchaguzi ukafanyika na akachaguliwa. Katiba ya nchi hiyo inatoa muda wa miaka 10 kwa kiongozi mmoja lakini kwa yeye miaka mitano haikutokana na kuchaguliwa, ndiyo maana aliruhusiwa na Mahakama,” alisema.
"Aliiongoza Burundi kwa miaka mitano uchaguzi ukafanyika na akachaguliwa. Katiba ya nchi hiyo inatoa muda wa miaka 10 kwa kiongozi mmoja lakini kwa yeye miaka mitano haikutokana na kuchaguliwa, ndiyo maana aliruhusiwa na Mahakama,” alisema.
Alifafanua pia kuwa usalama wa kila nchi ni muhimu
kwa mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hiyo ndiyo
maana wakuu wa nchi hizi walilaani mapinduzi hayo punde tu yalipofanyika
wakati wakuu hao wakikutana nchini.
Akifafanua kuhusu mchakato wa kusuluhisha pande
mbili zinazokinzana nchini humo, Membe alisema iwapo mawaziri
watashindwa kupata suluhu katika kikao kinachotarajiwa kufanyika,
watalazimika kumshauri Mwenyekiti wa EAC, Rais Jakaya Kikwete hatua
zaidi za kushughulikia amani ya nchi hiyo.
Hadi sasa makumi ya wananchi wameuawa tangu kuanza
kwa vurugu nchini Burundi huku maelfu ya wakimbizi wakikimbilia
Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni