Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia bibi mmoja ajulikanaye kwa majina ya Laurencia Athanas mkazi wa Kiseke, Ilemela jijini Mwanza kwa tuhuma za kumchoma visu vya moto mjukuu wake na kumsababishia majereha mbalimbali mwilini akimtuhumu kupoteza peni ya sh. 200.
Mtoto
huyo aitwaye Jackson Hosea ( 10 ) ambaye ni mwanafunzi wa
darasa la tatu katika shule ya msingi Kiseke iliyoko Ilemela
Jijini Mwanza alifanyiwa unyama huo nyumbani kwa bibi huyo
ambaye ni mzazi wa mama yake aishiye Nzega siku ya Ijumaa
jioni tarehe 23 May 2015.
Afisa
Mtendaji wa eneo hilo, Bi Hellen Mcharo ameithibitishia Mpekuzi
kutokea kwa tukio hilo na kudai kwamba liliibuliwa kwa mara
ya kwanza siku ya Jumatatu ya Mei 25, 2015 na mwalimu wa
mtoto huyo aliyemtaja kwa jina moja la Mwl. Midali
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni