Wananchi nchini Kenya wamemtaka mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambaye ni Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete kuingilia kati
mgogoro wa Burundi uliopelekea wanachi zaidi ya kumi kufariki dunia na wengine
kukimbilia nchini Tanzania.
Wakizungumza katika maandamano hivi karibuni ya kumpinga Rais
Nkurunziza kugombea tena urais raia hao wa Kenya wamemshinikiza Rais
Nkurunziza kusitisha mpango wake wa kugombea tena muhula mwingine ili
kuzuia machafuko yanayoendelea nchini Burundi hivisasa.
Hadi sasa takribani watu 18 wamefariki dunia kutokana na machafuko
hayo huku mahakama ya kikatiba ya nchi ikitangaza kumruhusu rais huyo
kuendelea kugombea kwa muhula wa tatu suala linalodaiwa kuwa kinyume na
Katiba ya nchi hiyo.
Aidha, Rais Pierre Nkurunziza amewatangazia wananchi kwamba endapo
atachaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo huo utakuwa muhula wake wa
mwisho.
Kwa upande mwingine Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki ameitisha mkutano na wakuu wa nchi za
jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam siku ya
Jumatano mei 13 kujadili mgogoro huo pamoja na Tanzania kutoa msimamo
wake dhidi ya Mgogoro huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni