Picha ikimwonyesha Norris kabla hajapata ajali, alivyopata ajali na baada ya kuwekewa uso mwingine wa marehemu |
Ajali nyingi duniani zimekua
zikisababisha vifo vya watu wengi huku zikiacha wengine wakiwa na
ulemavu wa maisha ambao huwasababishia kupoteza mwelekeo wa maisha yao
na kukata tamaa kabisa.
Pamoja na wengi kubaki na ulemavu,
lakini pia madaktari wamekuwa kijitahidi kadri wawezavyo kuwarudisha
watu hao katika hali zao lakini moja ya tukio la kushangaza ni la kijana
Richard Norris ambaye alipata ajali mbaya na kumpelekea kuharibika
vibaya sura yake.
Unaambiwa baada ya ajali hiyo
kijana huyo alishindwa kutoka nyumbani kwa takribani miaka 15 na amini
usiamini kijana huyo alifanyiwa upasuaji wa kihistoria uliochukua masaa
36 na kupandikizwa uso mpya wa mtu ambaye alishafariki baada ya kupata
ajali.
Upasuaji huo ulifanyika katika
hospitali ya University of Maryland Medical Center na ulifanikiwa kwa
kiasi kikubwa na sasa kijana huyo anaendelea vyema akiwa mwenye furaha.
Kwa kawaida kwa sababu ya maadili
ya utabibu watu waliopewa mabaki ya viungo vya wafu hawaruhusiwi
kukutana na jamaa au ndugu wa marehemu, lakini Norris hakuweza kujizuia
kukutana na Aversano, kutoka Maryland ambaye ni dada wa marehemu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni