Kila mwanamichezo au mwanamuziki hulipwa mshahara
kulingana na kiwango chake, hali hii ipo hivyo pia kwa waigizaji na watu
wengine wa kawaida.
Hali hii imekuwa ikiwapa morali zaidi wale
wanaofanya kazi kujituma ili wapate mshahara mkubwa zaidi au kupewa kazi
ya ziada tofauti na pale ulipozoea.
Hii pia imekuwa ikifanyika kwa wasanii wa filamu za Tanzania wenye
umoja wao maarufu kama Bongo Movies. Hao wamekuwa wakilipwa madau kama
wachezaji ili wafanye kazi za wenzao, hii imekuwa ikileta changamoto
kubwa kwa wasanii kuhakikisha wanapanda dau kutokana na uwezo binafsi.
Asilimia kubwa ya mashabiki wa filamu za kibongo wamekuwa wakitoa
fedha za kununua kazi zao bila kufahamu muhusika ‘anayemnunua’ amelipwa
kiasi gani cha fedha kucheza ‘movie’ aliyoinunua. Tazama bei zao hapa
chini:
Vincet Kigosi ‘Ray’
Inadaiwa kuwa
huyu jamaa ni mgumu sana kukubali kucheza filamu za watu. Alishawahi
kupewa Sh Milioni 10 ili cheze filamu moja (jina kapuni) lakini aligoma
na amekuwa na msimamo mkubwa katika kazi zake lakini badala yake hizo
fedha zikawalipa wasanii wengine watatu.
Inaaminika ndiye msanii
mwenye gharama kubwa licha ya kuwa mpaka sasa bado amekuwa akigoma
kucheza filamu za wenzake, ishu kubwa akidaiwa kujiona ni ‘staa’ zaidi
ya wenzake.
Wema Sepetu
Kipaji chake kiliibuliwa na
marehemu Steven Kanumba kupitia Filamu ya ‘A Point Of No Return’ baada
ya hapo akapata mashavu kibao na hadi sasa amefanikiwa kucheza filamu na
msanii mkubwa Van Vicker raia wa Ghana.
Wema Sepetu
Za mjini zinasema kabla
hajaachana na aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Clement alikuwa akitoza
kuanzia Sh Milioni Tano kwa filamu moja lakini sasa anapokea hata chini
ya hapo kwa kuwa fedha zimeanza ‘kumkatikia’.
Wema ambaye pia ni
Miss Tanzania mwaka 2006, alizaliwa mwaka 1988, Dar anamiliki kampuni
yake inayofahamika kama Endless Fame Films na ndiye mkurugenzi mtendaji.
Kajala Masanja
Ana kampuni yake ya uzalishaji
wa filamu inayoitwa Kay Entertainment na tayari ameshafanya kazi zake
zinayofahamika kwa majina ya Mbwa Mwitu pamoja na Pishu.
Lakini
linapokuja suala la kufanya kazi za watu inakulazimu kuzama katika pochi
au ‘waleti’ ukitoa mkono uwe na Sh Milioni Mbili lakini kwa kiasi hiki
awe anakufahamu na kama ‘ndo’ mnaona kwa mara ya kwanza jiandae kuachia
Sh Milioni Tatu hadi 2.5 zaidi ya hapo hakuna maneno maneno kazi
inapigwa kwa kiwango kikubwa tu na binti huyu aliyezaliwa mwaka 1983.
Jacqueline Walper ‘Wolper’
Ninja, dada mkubwa,
anaweza kucheza ‘sini’ zote ziwe za kijambazi, mke mwema na hata
changudoa, amekuwa na mashabiki wengi sana Bongo na hata nje ambao
wamekuwa wakipenda kazi zake.
Mshkaji huyu ambaye alizaliwa mwaka
1987 huko Moshi, Kilimanjaro, yupo kishkaji tu kwani anakubali kupokea
kuanzia Sh Milioni 2 hadi 2.5 hapo haipungui labda iongezeke ndipo
atakufanyia kazi zako. Mpaka sasa amecheza filamu zaidi ya 20.
Mzee Majuto
Licha ya kuzaliwa mwaka 1948 huko Tanga, Amri Athuman ‘King Majuto’ au
Mzee Majuto bado inaaminika kuwa ndiye msanii mwenye mashabiki wengi
zaidi Bongo kutokana na uimara wa kuigiza hususan kwenye filamu za
kuchekesha.
Mzee wa watu hana makuu ukitaka achekeshe weee filamu
nzima jiandae kumkatia Sh Milioni 1.5 hadi 2 tu, hicho ndicho kiwango
chake na atakufanyia kazi kwa umakini mkubwa zaidi ya hapo hashuki. Nje
ya fani anamiliki daladala mbalimbali huko kwao Tanga ambazo pia
zinamuongezea kipato.
Riyama Ally
Anaigiza kwa hisia kali sana katika
kila filamu, ukitaka alie na machozi yatoke kwa wingi au acheze filamu
za kimbea, majungu, vigodoro na nyinginezo wala hana makuu dada wa watu
anapokea hata Sh Milioni 1.5.
Riyama ambaye alianza kujihusisha na
maigizo mwaka 2000 akiwa na kundi la Taswira, mara nyingi katika filamu
alizocheza anasifika kwa kuigiza kwa uhalisia mkubwa pengine ukimtoa
Johari wa enzi za Tamthilia ya Johari basi huyu ni namba mbili kwa
wepesi wa kutoa machozi. Mpaka sasa amecheza filamu zaidi ya 40.
Blandina Chagula ‘Johari’
Alipata jina kupitia Tamthilia ya Johari kabla ya kuhamia kwenye
filamu. Ni Mkurugenzi wa Kampuni ya RJ akisaidiana na msanii mwenzake
Ray, katika kuindesha. Diva huyu wa movie za Kibongo alizaliwa mwaka
1983 huko Shinyanga.
Hana makuu katika kusaidia wenzake na mara
nyingi amekuwa akijitoa kwa moyo kucheza filamu yoyote. Dau lake ni la
ki-upendo zaidi kwani anapokea hata Sh Milioni Moja, hii yote anafanya
kwa lengo la kusaidia wenzake.
Anasifika zaidi kwa kucheza filamu za
kulialia kwani kwake kutoa machozi si lolote hata sekunde mbili hazipiti
anakuwa kayatiririsha hatari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni