Mgomo wa wafanyakazi wa mabasi yanayotoa huduma
jijini Dar es Salaam, leo asubuhi umesababisha mtafaruku mkubwa kwa
wakazi wa jiji hili ambapo wengi wao walionekana wakitembea kwa miguu
kuelekea kazini na katika shughuli zao mbalimbali.
Mgomo huo ambao unaenda sambamba na usafiri wa mabasi ya abiria nchi
nzima, unafuatia ule uliotokea Aprili 11 mwaka huu, ambapo wenye mabasi
na wafanyakazi wanataka maridhiano na serikali katika masuala
mbalimbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni