Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephati Gwajima amesema kwamba mwananchi au mwanasiasa yeyote asiyempenda Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akale limao
Askofu Gwajima alisema hayo juzi mara baada ya Edward Lowassa kumaliza
hatuba yake wakati akitangaza nia ya kutaka kugombea urais katika
uchaguzi mkuukwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, CCM.
Kabla ya kumaliza hotuba yake wananchi walimshinikiza Edward Lowassa
amsimamishe Askofu Gwajima ndipo Lowassa alimuita na kumpa maiki aongee
na wananchi waliofurika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.
Askofu Gwajima alianza kwa kuomba mwenyezi Mungu aibariki safari ya
Matumaini ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa na mwisho kabisa
kuwapa mjumbe mzito wananchi kuwa mwenye Chuki na Lowassa akale limao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni