Filikunjombe akifurahi kwa kupinga ngoma na wanafunzi wa shule ya msingi Mavanga
Filikunjombe akicheza na wanafunzi wa Mavanga Sekondari
Filikunjombe akiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa Mavanga Sekondari
Mmoja wa wanafunzi wanaolipiwa ada na Filikunjombe shule ya sekondari ya Mavanga akimshukuru mbele ya wazazi na wanafunzi wenzake
Filikunjombe akipewa zawadi na baadhi ya wanafunzi anaowalipia Ada
Mpango wa
mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe kupitia chama cha mapinduzi Mh.Deo
Filikunjombe wa kuwalipia ada za shule za Seokondari wanafunzi 25 kwa kila kata
umefanikiwa kwa kiasi kikubwa hivyo kuwafanya wananchi wa jimbo hilo kuukubari
na kumuomba kuendelea na utaratibu huo ambao umeweza kuwanufaisha wanafunzi
walio wengi wanaotoka katika mazingira magumu.
Mmoja wa
wananchi wa kata ya Mavanga Bw.John Haule alisema kuwa awali kabla ya
Filikunjombe kuingia madarakani watoto yatima walitegemea sana mashirika yasio
ya kiserikali kuwasaidia katika kulipia gharama za masomo lakini haikusaidia
lolote kwani mashirika yaliyo mengi hupata ufadhiri kwa miaka michache na
miradi hiyo inapikwisha hali ilibaki kuwa mbaya kwa watoto hao tofauti na
kipindi hiki.
Bw.Haule
alisema kuwa tokea alipoingia madarakani Filikunjombe ndani ya miaka mitano
ameweza kuwalipia ada wanafunzi ambao wamefanikisha kuhitimu masomo yao kwa
ngazi ya kidato cha nne na waliofanikiwa kufaulu ameendelea kuwapa msaada kwa
kuwalipia ada katika ngazi ya kidato cha tano.
Alisema
wilaya ya Ludewa yenye kata 26 wameweza kusaidiwa zaidi ya wanafunzi 700 ambao
mpaka sasa kuna wengine wameweza kujiunga na fani mbalimbali za ufundi baada ya
kuhitimu kidato cha nne lakini kubwa zaidi wamekuwa wakikumbuka mchango wa
mbunge wao katika maisha yao kwa kumpokea kwa shangwe na kumpa zawadi
mbalimbali pale anapotembelea vijijini hali ambayo imemtia moyo mbunge huyo na
kuona mpango wake umefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
“Mpango wa
Filikunjombe umefanikiwa kwa asilimia miamoja kwani tumeanza kuyaona matunda
yake lakini wakati anaanza na mpango huu wa kuwalipia ada wanafunzi wa
mazingira magumu kwa kuwaagiza viongozi wa kata na vijiji kupendekeza majina ya
watoto tuliona kama ni siasa leo hii kila mmoja wetu ameona faida yake hivyo
tunamuomba aendeleze mpango huu kwani ni ikombozi wakielimu katika wilaya yetu”,alisema
Bw.Haule.
Katibu wa Itikadi
na uenezi wa chama cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Njombe Bw.Onoratus Mgaya katika
ziara ya mbunge huyo kata za Mavanga,Ngelenge,Mawengi na Lupanga alisema kuwa
chama cha mapinduzi kina hazina ya viongozi wachapa kazi akiwemo Filikunjombe
hivyo wananchi wanapaswa kutambua umuhimu wa kuwaunga mkono vingozi wa namna
hiyo.
Bw.Mgaya
alisema licha ya kuwalipia ada za shule watoto wa mazingira magumu pia
Filikunjombe amekuwa ni mfano wa kuigwa nchini kwa kutekeleza ilani ya chama
cha mapinduzi katika jimbo lake kwa muda muafaka hali ambayo imekuwa ikikipa
sifa chama na kuwafanya wananchi kuendelea kukipa nafasi ya kuendelea kushika
dora miaka mingi ijayo.
Akihutubia
katika mkutano wa hadhara kwa wananchi wa kata ya Mavanga Bw.Mgaya alisema kuwa
CCM sio chama kibaya kamabaadhi ya wanasiasa wengine wanavyosema ila kunawatu
wako ndani ya ccm ni wabaya na mkakati wa chama ni kuwaondoa watu hao haraka
iwezekanavyo ili kusikiliza vilio vya wananchi kwani wananchi wanahitaji
maendeleo na si porojo.
Aidha
akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mavanga Filikunjombe alisema
kuwa mpango wake wa kuwalipia ada wanafunzi ulikuwa wa majaribio lakini kabla
haja fanya utafiti wa majaribio yake ameshayaona mafanikio makubwa ambayo
hakuyatarajia kutokana na kila kijiji anachopita amekuwa akipata mapokezi
makubwa na zawadi kwa baadhi ya wanafunzi aliyowasaidia.
Filikunjombe
alisema licha ya kutoa msaada huo wa wanafunzi wenye mazingira magumu pia
amekuwa akiwasisitiza wazazi kuwapeleka watoto shule ili mwisho wasiku waje
kuwa viongozi wa wilaya hiyo kwani yeye si mbunge wa milele katika jimbo la
Ludewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni