Jumapili, 12 Aprili 2015
Ajali ya basi la abiria na lori la Fuso Ruaha Mbuyuni leo
Habari
zilizotufikia punde zinasema watu kadhaa ambao idadi yao bado
haijafahamika wanasemekana wamepoteza maisha baada ya basi la abiria
liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero
kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo
kuteketea kwa moto maeneo ya milimani kilomita kadhaa kutoka Ruaha
Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya saa mbili asubuhi leo. Pichani ni
basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Picha ya Fuzo
bado haijaletwa. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizi na tutazileta mara
zitapopatikana.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni