Jumatano, 8 Aprili 2015

Uganda yawakamata washukiwa wa Mauaji


 
Uganda inasema imekamata watu kadhaa kuhusiana na mauaji ya mwendesha mashtaka Joan Kagezi yaliyotikea wiki iliopita.
Uganda inasema imekamata watu kadhaa kuhusiana na mauaji ya mwendesha mashtaka Joan Kagezi yaliyotokea wiki iliyopita.
Mwendesha mashtaka huyo aliuawa na watu waliokuwa na bunduki wakitumia pikipiki na polisi kuanza uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo.
Tangu kuuawa kwa mwendesha mashtaka huyo wiki iliopita polisi imekuwa katika tafuta tafuta ya wale waliofanya kitendo hicho na hadi sasa haijaweza kupata nani anaehusika haswa,

lakini leo polisi inasema huenda imepata fununu.
Polisi walizingira nyumba moja katika kiunga cha jiji la Kampala sehemu za Kyengera katika barabara kuu ielekeayo kusini magharibi mwa nchi.
Mkuu wa polisi Generali Kale Kaihura alifika mahali hapo na kuielezea BBC kuwa walikuwa wanatekeleza msako baada ya kupata fununu zinazowahusisha wenye nyumba hiyo na matukio ya utovu wa usalama.
Watu waliokamatwa hapo wanafikia watano wanaume wawili na wanawake watatu kutoka mahali hapo.
Kutokana na matukio ya kigaidi katika nchi jirani Kenya polisi ya Uganda imekuwa chonjo kama anavyofafanua mkuu wa polisi ya Uganda.
Kutokana na matukio ya kigaidi katika nchi jirani Kenya polisi ya Uganda imekuwa chonjo
Licha mkuu wa polisi kukataa kufafanua wangapi wamekamatwa lakini duru za kuaminika zinasema awalikamtwa watu watano ambapo wawili ni wanaume na watatu wanawake lakini duru hazikufafanua zaidi.
Kukamatwa kwa watu hawa kunakuja siku chache baada ya taarifa kutokea zikienysha kama polisi inamshikilia mwanaume mmoja ambaye alikuwa anapiga picha bweni moja karibu na chuo kikuu cha Makerere mjini Kampala.
Hakuna maelezo zaidi kuhusu kisa hicho.
Ila marehemu Joan Kagezi, mwendesha mashtaka aliyepigwa risasi wiki iliopita alizikwa mwishoni mwa juma nyumbani kwake.
Bado haijabainika nia ya waliompiga risasi ilikuwa nini.
Marehemu alikuwa anaongoza kesi dhidi ya washukiwa 13 ambao wanashtumiwa kuhusika na utegaji mabomu yaliowauwa watu zaidi ya 70 mjini Kampala mwaka wa 2010 katika ukumbi wa kutizama kandanda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa