Baba
mmoja India amefikia uamuzi wa kuuza figo yake ili kupata pesa za
matibabu ya watoto wake ambao wana tatizo la kuwa na uzito mkubwa.
Watoto
hao ambao wa kwanza ana miaka mitano uzito wake ni kg.48, wa pili
anamiaka mitatu uzito wake ni kg. 34 na wa mwisho ana miezi 18 na uzito
wake ni kg. 15, ni miongoni mwa watoto walioweka historia duniani
kutokana na kuwa na uzito mkubwa.
Wazazi
wao wamesema wamekuwa wakipata wakati mgumu wa kuwahudumia watoto hao
chakula kutokana na kula chakula kingi, kwa wiki wanakula chakula
kinachotosha kuliwa na familia mbili kwa mwezi mzima.
Baba
huyo ana hofu kuwa kama watoto wake wataendelea na hali hiyo huenda
wakapoteza maisha kwa siku za baadaye, kaona atafute mteja wa kumuuzia
figo yake moja ili apate hela kuwapeleka watoto hao kwa mtaalamu
atakayewasaidia.
Kwa siku watoto hao wawili Yogita na Anisha kawaida wanakula chapati 18, wali kilo tatu, mifuko sita ya crips, maboksi matano ya biskuti na ndizi 12.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni