Jana kupitia mitandao wa Instagram msanii Mabeste alielezea hali ya kiafya ya mkea wake na kuomba msaada wa kuchangiwa ili aweze kuendelea na matibabu.. taarifa zimemfikia Soudy Brown kuwa ndugu wa upande wa mke wake wamepinga kitendo hicho..
Soudy kaongea na dada yake anayeitwa Leyla,
amesema ni kweli mdogo wake anaumwa sana na anaendelea na matibabu
ingawa kuhusu suala la kumchangia kama familia hawakukaa na kuzungumza
wala hawakuhusishwa chochote walishangaa kuona taarifa hizo.
Dada huyo amesema familia baada ya kuona
hali ya ndugu yao imezidi kuwa mbaya wakashauriana apimwe vipimo vyote
wakati anaendelea na vipimo wakashangaa kuona taarifa hizo kwenye
mitandao ingawa ni kweli anahitaji msaada kutokana na kuugua kwa muda
mrefu ila kama familia hawakuhusishwa chochote, Mabeste amemuuguza peke yake kwa muda mrefu, lakini wao kama familia hawajawahi kumchangia kwa sababu walijua Mabeste ana fedha za kumuuguza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni