Ijumaa, 17 Aprili 2015

WANANCHI WAJITOLEA KUCHIMBA NGUZO KUPELEKA UMEME MANDA

Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo akichimba mashimo ya nguzo za umeme unaoelekea Manda
Katibu wa vijana wa CCM Bw.Menrad Mtega akitoka kuchimba shimo






Mwandishi wa mtandao huu Nickson Mahundi mwenye laba akiwa na mh.Mchilo katikati pamoja na muhandisi wa mradi huo Fredrick Mathia
Muhandisi wa mradi akiwajibika

Huyu ndyiye muhandisi wa mradi 



Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Lusiano Mbosa akiwajibika

 Kazi na dawa diwani akichoma mahindi kwani njaa tayari

Wananchi wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameshauliwa kuendelea kudumisha dhana ya kujitolea katika kazi mbalimbali ili kujiletea maendeleo haraka kwani mipango ya Serikali ni ya muda mrefu hivyo huchelewa kutekelezwa kwa muda muafaka kutokana na halihalisi ya bajeti ya Serikali kutokana na hali hiyo wananchi yameanza kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kuelekea kata ya Manda.
Hayo yamesemwa leo na Diwani wakata ya Ludewa mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM)Mh.Monica Mchilo wakati akifanya kazi uchimbaji wa mashimo ya kusimika nguzo za nishati ya umeme katika mtaa wa Ngalawale ambapo wananchi kwa kushirikiana na vingozi mbalimbali wameungana na wataalamu wa umeme kukamilisha zoezi hilo la ujenzi wa njia ya umeme kuanzia Ludewa kijijini  hadi kata ya Manda pembezoni mwa ziwa nyasa.
Mradi huo wa Umeme ambao unafadhiriwa na Wakala wa nishati ya umeme vijijini(REA) kwa awamu ya kwanza utaanzia Ludewa kijijini kuelekea maeneo ya Ngalawale,vijiji vya Kimelembe,Nkomang’ombe,Luilo,Lifua na Kipangala na awamu ya pili utapita vijiji vya Lihagule,Masasi,Kipingu,Ngelenge,Ilela,Nsungu,Igalu na Mbongo.
Mh.Mchilo alisema wananchi wanapaswa kujitolea katika kazi mbalimbali ili kujiletea maenteleo kwa haraka pale wanapoona tayari Serikali imeingiza mkoano wake kwani kumekuwa na dhana potofu ya baadhi ya wanasiasa kuwakatisha tama wananchi wakiwataka wabweteke na kuisubiri Serikali ifanye kila jambo hali ambayo si sahihi.

“Nawapongeza wananchi kwa kuamua kuanza kwa nguvu zenu kuliko mngeisubiri Serikali iwafanyie kila jambo na huu ndio urithi aliyotuachia baba wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kama watanzania wangelitambua hili linalofanywa wilayani Ludewa na kulitendea kazi basi kila kijiji na wilaya nchini kusingekuwa na malalamiko ya kuilaumu Serikali”,alisema Mh.Mchilo.

Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM)wilaya ya Ludewa Bw.Lusiano Mbosa alisema kuwa  katika suala la maendeleo hakuna siasa hivyo aliwataka wananchi kuendelea kujitolea kuchimba mashimo ya nguzo za umeme bila kuwasikiliza wapinga maendeleo kwani umeme huo utawanufaisha wananchi na si wapinga maendelea.
Bw.Mbosa alisema kuwa ifike wakati siasa zikae kando kwani tayari Serikali kupitia REA  imeshatoa fedha za mradi huo wa umeme hivyo kila mwananchi anapaswa kuhusika na uletwaji wa jambo hilo la kimaendeleo ambalo litakinufaisha kizazi kilichoko na kijacho.
Aidha msimamizi wa mradi huo wa ujenzi wa njia ya Umeme kutokea kata ya Ludewa hadi kata ya Manda kutoka kampuni ya Power Magics Bw.Fredrick Mathia alisema katika mradi huo anakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa barabara katika msimu huu wa mvua hivyo magari yanayobeba nguzo kukwama katika tope.
Bw.Fredrick alisema kuwa mpaka sasa kuna baadhi ya vijiji tayari nguzo zimeshafika lakini bado kiasi kikuba cha nguzo hazijaletwa kwani mradi huo unatekelezwa kwa muda wa miezi mitatu lakini kutokana na hali halisi utachelewa kukamilika kwa wakati.

Alisema ameshangazwa na umoja wa wananchi wa wilaya ya Ludewa kwa kujitolea kuchimba mashimo ya nguzo za umeme tofauti na maeneo ambayo amewahi kufanya kazi hali ambayo ni mfano wa kuingwa kwa wananchi wengine nchini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa