Jumanne, 28 Aprili 2015

Yanga waingia kambini kujiandaa na Etoile


Mabingwa wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara, Young Africans, wameingia kambini kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora dhidi ya Etoile du Sahel.
Akizungumza na East Africa Radio, mkuu wa kitengo cha mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema, wanatarajia kuondoka wakiwa na msafara wa watu 50 kukiwa na viongozi, wachezaji na benchi la ufundi wakiwa sambamba na mashabiki watakaokuwa wakiwapa sapoti katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii nchini Tunisia.
Muro amesema, mpaka sasa hakuna majeruhi katika kikosi hicho na wanaamini watafanya vizuri katika mchezo huo na hatimaye kuingia katika hatua ya nane bora hatua wanayoamini watakwenda nayo vizuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa