Mtoto mwenye umri wa miaka 05
aliyetambulika kwa jina la Jonson Mwamwere, mkazi wa Nsalaga jijini
Mbeya, aliuawa kwa kupigwa sululu kichwani na kutenganishwa kichwa na
kiwiliwili na mjomba wake aitwaye Yona Mwamwere.
Kwa Mujibu kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Ahamed Msangi, Mwamwere alikuwa anamfukuza mtoto huyo na
alikimbilia kwenye jengo lililopo jirani na nyumbani kwao ambalo bado
lipo kwenye ujenzi na alipofika kwenye jengo hilo alimuua mjomba wake
huyo kwa kumpiga kichwani kwa sululu na kutenganisha kichwa na
kiwiliwili
Kamanda Msangi amesema kufuatia tukio
hilo mafundi waliokuwa wakiendelea na ujenzi walipiga kelele za kuomba
msaada, hivyo kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi
walijitokeza na kumshambulia mtuhumiwa kwa kumpiga hadi kufa na kisha
kuuchoma moto mwili wake.
Marehemu wote walikuwa ni ndugu
wanaoishi nyumba moja, miili yao imehifadhiwa hospitali ya rufaa Mbeya
na chanzo cha tukio hili kinachunguzwa ingawa uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa marehemu Yona alikuwa na matatizo ya akili.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe
16.03.2015 majira ya saa 11:00 asubuhi huko katika mtaa wa
nsalaga-uyole, kata ya nsalaga, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni