Mawakili wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, wameandika barua kuliomba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuandika kimaandishi nyaraka wanazozihitaji azipeleke pamoja na vifungu vya sheria vinavyomtaka awasilishe nyaraka hizo.
Barua
hiyo iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala iliwasilishwa jana mchana
katika jeshi hilo, ikiwa ni siku moja baada ya jeshi hilo kumtaka Askofu
Gwajima kuwasilisha nyaraka 10, Aprili 16 mwaka huu watakapoendelea na
mahojiano.
Gwajima
aliitwa kuhojiwa na jeshi hilo mara mbili kutokana na kufunguliwa
jalada la malalamiko ya kumkashifu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo
Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Katika
barua hiyo, mawakili hao kwa niaba ya mteja wao wanaliomba jeshi la
polisi kumwandikia barua rasmi kimaandishi, Gwajima wakiainisha nyaraka
wanazozihitaji pamoja na vifungu vya sheria vinavyotumika na jeshi hilo
kutaka nyaraka hizo.
Mawakili
hao wanasema watashukuru kupata hati hiyo ambayo hawaijui jina lakini
wanaamini jeshi la polisi litafahamu jina la kisheria la nyaraka husika
inayotumika kumtaka Gwajima awasilishe nyaraka wanazozihitaji.
Aidha wanasema Askofu Gwajima atakapopata nyaraka anayoihitaji atatimiza wito na kuchukua hatua stahiki za kisheria.
Mpekuzi blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni