Jumanne, 21 Aprili 2015

Raia afanikisha kuzuia waliopora na kujaribu kutimua




Watu kadhaa wametiwa chini ya ulinzi katika mataa ya Red Cross jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa kuvamia na kumpora mzungu fedha huko Kinondoni karibu na beni ya Stanbic.

Raia aliyeshuhudia tukio hilo aliwakimbiza kwa gari na kufanikiwa kuwazuia (block) na askari wa doria wakawatia mbaroni wakiwa na bunduki mbili.
Sehemu ya ujumbe kuhusu tukio hili, uliopatikana via WhatsApp unasema, "kuna jamaa alijitolea kuwafuata nyuma nyuma mpaka hapo redcross kwenye taa ndio akawaa block coz kuna askari, jamaa walipo-blockiwa wakashuka na mitutu, askari wa pikipiki wakawaweka chini ya ulinzi fasta."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa