Chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania, TABOA kimesema mgomo wa madereva unaotarajiwa kuanza kesho ni batili.
Sababu kubwa ya madereva hao kugoma ni kuishinikiza serikali kuweka mfumo mzuri wa ajira na kupinga kanuni inayowataka kurudia kusoma katika chuo cha taifa cha usafirishaji,NIT kila leseni zao zinapokwisha muda.
Kwa
mujibu wa TABOA, madereva waliopanga kugoma hawatambuliwi
kisheria,kwani wapo waliofukuzwa kazi kutokana na sababu
mbalimbali ikwamo kusababisha ajali na sasa hawana magari ya
kuendesha.
Mwenyekiti
wa TABOA Mkoa wa Dae es Salaam, Hamza Mringo alisema madereva
wanaotambuliwa kihalali na mamlaka ya usafirishaji Nchi kavu
na majini,SUMATRA hawajawahi kushiriki mgomo uliofanyika April
mosi, na hawatashiriki kamwe.
"Madereva
wetu hawawezi kugoma kwa sababu tunaamini kila kitu kinaamriwa
kwa utaratibu,tumepanga kukutana na serikali tuone jinsi ya
utekelezaji wa hiyo kanuni inayoleta shida.
"Baada
ya kuongea na serikali tukaelewana,tutakuwa tayari kuwalipia
madereva wetu kozi ambazo wao wanaziona ni kero...inaelekea
mgomo huu unamkono wa mwanasiasa mmoja tunamjua," alisema.
"Wao wana ajenda yao ya siri,sisi hatutaki magari yetu yatumike kama ngao ya kutugombanisha na serikali.
"Mbaya zaidi hizi vurugu zao wanataka kuzifanyia eneo letu la kazi ambalo tumekabidhiwa kihalali." Alisema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni