Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amesema anashindwa kujitokeza kuzungumzia au kufanya mambo yanayohusiana na urais kwa kuwa Kamati ya Maadili ya CCM inamfuatilia kwa karibu.
Alisema hayo
jana alipoulizwa kuhusu kauli ya Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita
akiwa Marekani ambako alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana
nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10.
Kikwete
alisema: “Wakati unaingia Ikulu unakuwa na shauku kubwa pamoja na furaha
ya ushindi, lakini hakika urais ni kadhia kubwa. Ukipata fursa ya kuwa
rais kwa awamu mbili kama mimi nadhani zinatosha kabisa. Nimefanya mengi
kwa nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia.”
Kauli
ya Lowassa inakuja ikiwa ni siku chache baada ya makada wengine
wanaotajwa kuwania urais kupitia CCM kueleza maoni yao juu ya kauli hiyo
ya Rais.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba alisema kuwa kauli hiyo
inampa hamasa kwa nia yake ya kutaka kuwania urais na kwamba alitangaza
nia hiyo huku akifahamu kwa asilimia 100 uzito wa jambo hilo akisema
kufahamu changamoto hizo ndiyo moja ya vitu vilivyomsukuma kuchukua
uamuzi huo.
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye
alisema: “Kama mtu ameamua kuwania nafasi hiyo ina maana anafahamu
anachokitaka. Tunajua ziko changamoto na namna ya kukabiliana nazo, kwa
hiyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.”
Mbunge wa
Nzega, Dk Hamis Kigwangalla alisema: “Kauli kama hiyo haiwezi kumvunja
mtu moyo, ari itabaki palepale tu kwa aliyetangaza nia. Aliyetangaza nia
anataka kutoa utumishi wake kwa nchi yake kama mimi.”
Lowassa hajatangaza wazi nia hiyo zaidi ya kusema ameshawishika
kuwania urais baada ya hivi karibuni, makundi mbalimbali kufika nyumbani
kwake mjini Dodoma kumshawishi achukue fomu kuwania nafasi hiyo.
Miongoni
mwa makundi yaliyojitokeza na kumshawishi pamoja na kumchangia fedha za
kuchukua fomu ya kugombea urais ndani ya CCM ni pamoja na masheikh
kutoka wilayani Bagamoyo, wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste,
wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na madereva bodaboda.
Msimamo wake hadi jana
Akizungumza
jana wakati wa kuaga mwili wa Mkurugenzi wa zamani wa Mamlaka ya Hali
ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Mohamed Mhita nyumbani kwa marehemu Oysterbay
jijini Dar es Salaam, Lowassa alisema:
“Muda mwafaka ukifika nitatangaza nia na kuweka mikakati yangu wazi ili wananchi waijue. Kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu ninatazamwa sana na chama.
"Ninachoweza kusema, siku nitakayotangaza nia, nitaeleza ni nini nitafanya kukabiliana na changamoto zote zilizopo Ikulu.
“Muda mwafaka ukifika nitatangaza nia na kuweka mikakati yangu wazi ili wananchi waijue. Kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu ninatazamwa sana na chama.
"Ninachoweza kusema, siku nitakayotangaza nia, nitaeleza ni nini nitafanya kukabiliana na changamoto zote zilizopo Ikulu.
“Ninafahamu
kuna changamoto nyingi, lakini siwezi kusema, subirini siku
nitakapotangaza nia, nitaelezea ni kwa namna gani nitakabiliana na
changamoto zilizopo katika ofisi hiyo nyeti nchini.”
Waziri
mkuu huyo wa zamani, ni mmoja kati ya makada wa CCM ambao wameonyesha nia
ya kutaka kumrithi Rais Kikwete katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika
Oktoba na pia ni miongoni mwa makada sita wa chama hicho waliokuwa
wamefungiwa kwa miezi 12 na kamati kuu kwa kufanya shughuli
zinazoashiria kufanya kampeni mapema.
Wana-CCM wengine
waliotangaza nia na wanaotajwa katika kinyang’anyiro hicho ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Stephen Wasira, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe, Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi,
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni