Ijumaa, 10 Aprili 2015

LUDEWA QUEENS FC WAMPONGEZA FILIKUNJOMBE



Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monica Mchilo akikabidhi vifaa vya michezo mwalimu wa timu ya mpira wa miguu timu ya wasichana Ludewa Queens 

Wachezaji wa timu ya Ludewa Queens

Hawa ndiyo viongozi wa chama cha mpira wilaya ya Ludewa pamoja na viongozi wa Ludewa queens pamoja na Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo
Mh.Mchilo akiwa na timu ya Ludewa Queens
Mh. Diwani  Kata ya Ludewa Bi. Monica Mchilo akipokea taarifa kutoka kwa viongozi watimu
Wachezaji wakiwa katika sare walizopewa na Mbunge

Mh.Mchilo akiwa na timu ya mpira wa miguu Ludewa queens
 Diwani wa kata ya Ludewa Mama Monika Mchilo

Timu ya mpira wa miguu ya wasichana wilayani Ludewa ijulikanayo kwa jina la Ludewa queens fc imempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe kwa kuisaidia timu hiyo katika mambo mbalimbali likiwemo la kuwawezesha kusafiri kwaajili ya michezo ya majaribio na wilaya nyingine pia kwa kuipatia vifaa vya michezo mara kwa mara.

Akiongea katika hafla iliyoandaliwa na uongozi wa timu hiyo ya kuwakutanisha na wadau mbalimbali wa mchezo wa mira wa miguu upande wa wasichana mwalimu wa timu hiyo Hilaly Lugome alisema timu hiyo imekuwa ikipata mafanikio mbalimbali kutokana na Mbunge huyo kujitolea katika mambo mbalimbali likiwemo la vifaa vya michezo na usafiri hasa gharama za mafuta wanapotaka kusafiri.

Mw.Lugome alisema wachezaji wa timu hiyo mpaka sasa wameweza kushiriki katika mshindano mbalimbali ikiwemo ligi ya taifa kwani waliweza kuunga na wezao wa Njombe na kuuwakirisha mkoa wa Njombe katika Ligi hiyo na kutolewa  kwa kipigo cha gili moja na kushindwa kuendelea na mashindano hayo ya Taifa.

Alisema katika mshindano hayo ambapo wachezaji wengi wa timu ya mkoa wa Njombe walitoka katika timu ya Ludewa Ludewa Queens fc baadhi yao wachezaji watano walichaguliwa ili kufanyiwa majaribio katika timu ya wasichana ya taifa Twiga stars hivyo bado wanajifua kwa kusubiri kuitwa katika majaribio hayo.

“Tunamshukuru Mbunge wetu Filikunjombe kwa mchango wake katika tumu yetu pia Mama Monika Mchilo Diwani wa kata ya Ludewa Mjini ambaye ni mlezi wa timu yetu na wadau wengine kama Bw.Augustino Lugome ambaye ni mwananchi wa kata ya Luana kwa kutupatia sale aina mbili na mipira miwili tunawaomba kuendelea na moyo huo ili kuendeleza michezo wilayani Ludewa”,alisema Mwl.Lugome.

Akizungumza kwa niaba ya Mh.Deo Filikunjombe Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo ambaye ni mlezi wa timu  alisema timu hiyo imekuwa ni timu ya kwanza katika timu za mpira wa miguu wasichana kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali hivyo haina sababu ya kukosa misaada kwa wadau wa soka wilayani Ludewa.

Alisema awali wakati akiombwa kuwa mlezi wa timu hiyo alisita lakini kutokana na umahili wa mabinti wanaochezea timu hiyo wawapo uwanjani ailimpasa kukubali wito huo na kuendelea kuisimamia hivyo yeye alitoa jezi aina mbili na mipira miwili kwaajili ya mazoezi.

Mh.Mchilo alisema kuwa Filikunjombe alimtuma kuwasikiliza matatizo ya tumu lakini yeye kama mlezi anayajua hivyo atamfikishia mbunge ili aendelee kuwasaidia katika yale yanayowezekena kwa kipindi hiki kwani kunatimu nyingi za mpira wa miguu za wananume zimepereka maombi ya vifaa vya michezo kwa mbunge huyo.

Aidha mh.Mchilo amewapongeza wadau mbalimbali akiwemo Augustino Lugome ambaye ameonesha kuiunga mkono timu hiyo hivyo aliwataka wadau wengine kuiga mfano huo ili kuendeleza mchezo huo kwa wanawake.

Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa