Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amezindua meli mbili kubwa za kisasa za kivita
zenye meta 60, mizinga mikubwa miwili na ya kawaida sita kila moja, na
uwezo wa kupiga makombora umbali wa kilometa saba angani na kilometa
tisa chini ambazo zitakazowezesha usalama wa
uhakika katika ukanda wa bahari wa Tanzania dhidi ya maharamia.
uhakika katika ukanda wa bahari wa Tanzania dhidi ya maharamia.
Mara baada ya uzinduzi Rais. Kikwete amezikabidhi kwa kamandi ya
jeshi la wanamaji hafla iliyofanyika makao makuu ya kamandi hiyo
yaliyopo kigamboni jijini Dar es salaam ambapo amesema meli hizo
zinafanya Tanzania iandike historia mpya ya kuwa na meli kubwa na za
kisasa kwa mara ya kwanza nchini.
Akizungumza katika uzinduzi huo waziri wa ulinzi na jeshi la
kujenga taifa,Dk.Hussein Mwinyi, amesema, meli hizo zitakuwa tegemeo
kubwa katika kulinda eneo la maji ya tanzania na rasilimali zake ikiwamo
gesi asililia,samaki kwani zina uwezo wa kasi kubwa katika kukabiliana
na vitendo vya uhalifu hasa uharamia.
Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usama nchini, Jenerali Davis
Mwamunyange, amesema,lengo la kuwa na meli za jinsi hiyo ni katika
jitihada za kuhakikisha jeshi linakuwa na silaha za kisasa za kivita na
kutoa mafunzo huku balozi wa china nchini, Lui Youging, akimpongeza Rais
Kikwete kwa jitihada za kuimarisha ulinzi wa taifa lake.
Meli hizo zimepewa majina ya melivita P77 Mwitongo kuwakilisha eneo
alilozaliwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere na
melivita P78 Msoga, eneo alilozaliwa Rais Kikwete ambaye anatarajia
kumaliza kipindi chake cha uongozi Novemba mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni