Haya ni baadhi ya matairi ya magari yaliyochomwa na baadhi ya Wananchi
maeneo ya stendi kuu ya Ubungo jijini Dar. Polisi wametumia mabomu ya
machozi kuwatawanyisha wananchi hao.
Baadhi ya Wananchi
hawakukubaliana na hilo nao wakaanza kushika mawe na kuwarushia Polisi, ikawa
ni mawe VS Mabomu. Haya yote chanzo ni mgomo wa Madereva ulioanza leo.
Mpekuzi blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni