Jumatano, 29 Aprili 2015

Mahakama Kuu Kenya Yakubali Ombi La Vyama Vya Mashoga Kusajiliwa


Katika hatua ya kushitua, Mahakama Kuu nchini Kenya imesalimu amri mbele ya mashinikizo ya watetezi wa vitendo vichafu vya ulawiti, usagaji, ushoga na kusema kuwa sasa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uasherati wanaweza kusajili mashirika ya kile kinachodaiwa ni kutetea haki zao za kibinadamu.
 
Majaji watatu wa mahakama hiyo wameiamuru Bodi ya Kusimamia Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kulitambua na kulisajili shirika moja ambalo awali mahakama hiyo ilizuia lisajiliwe kwa sababu za kimaadili na kidini.
 
Jopo hilo la majaji Isaac Lenaola, Mumbi Ngungi na George Odunga limedai kuwa, katiba ndio marejeo ya kila kitu nchini Kenya na kwamba serikali haitakiwi kuzingatia mafundisho ya kidini katika maamuzi yake ambayo kwa mujibu wa majaji hao, maamuzi hayo yananyima kundi fulani la watu uhuru wao.
 
Uamuzi huo umechukuliwa huku mashinikizo ya nchi za Magharibi dhidi ya nchi za Afrika ya kuzitaka zitambue rasmi vitendo hivyo vichafu yakizidi kupamba moto.
 
Nchi za Magharibi yametishia kuzinyima misaada nchi za Afrika iwapo hazitatambua rasmi vitendo vya ulawiti na usagaji.
 
Hatua ya Mahakama Kuu ya Kenya imechukuliwa pia katika wakati huu wa kukaribia ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini Kenya ambaye ni mtetezi mkuu wa vitendo hivyo vichafu.
 
CHANZO: IRAN SWAHILI
Mpekuzi blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Jumla ya Mara Iliyotazamwa