Alhamisi, 30 Aprili 2015

Kijana aokolewa akiwa hai Nepal


Kijana aokolewa siku tano baada ya kufunikwa na kifusi
Watoa huduma za uokoaji huko mji mkuu wa Nepal Kathmandu, wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya funikwa na vifusi vya jengo

Yanga kuibeba Simba CAF?


BAADA ya watani zao wa jadi Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu vita ya kuwania kushiriki michuano ya kimataifa sasa mwakani imesalia kwa vigogo wengine wa soka nchini Simba SC na Azam FC.

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamuduni na Michezo, Dk. Fennela Mukangara Kuikabidhi Yanga kombe


WAZIRI wa Habari, Vijana Utamuduni na Michezo, Dk. Fennela Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi Kombe la Ubingwa

TFF Yatembeza Adhabu kali Ligi Kuu


MWAMUZI wa mechi kati ya Azam FC na Kagera Sugar, Stephen Makuka na msaidizi wake namba mbili Said Mnonga wameondolewa kwenye orodha za waamuzi wa Ligi Kuu na kufungiwa kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kushindwa kumudu mchezo huo.

Mwanafunzi auawa baada ya kukutwa na barua ya mapenzi


MWANAFUNZI wa Kidato cha Pili, Jofrey Robert Mwakatenya (15) anatuhumiwa kuuawa kikatili na baba yake mzazi, Robert Mwakatenya (35) baada ya kumkuta akiwa na barua ya mapenzi, inayodaiwa aliandikiwa na rafiki wake wa kike.

Msajili Avionya Vyama Vya Siasa....Avitaka Viache Siasa Za CHUKI ili Kuepusha Machafuko Ya Kisiasa


MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevionya vyama vya siasa na wanasiasa wasikamiane na kukomoana kwa sababu, kufanya hivyo hakujengi demokrasia wala kuisaidia nchi.

Mbunge Bahi , Omary Badweli, Ashinda Kesi ya Kuomba RUSHWA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Mbunge wa Jimbo la Bahi mkoani Dodoma, Omary Badweli, aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya

Kaseja, Mgosi Wagoma Kurudi Simba


WAKATI kukiwa na tetesi za Simba kutaka kuwarudisha kundini wachezaji wake wa zamani Juma Kaseja na Mussa Hassan ‘Mgosi’ ili kuimarisha kikosi chao

Sarafu ya Sh 500 YAHUJUMIWA....... Yanunuliwa kwa Sh. 2500 hadi 5000 ili Kutengeneza Mikufu, Benki Kuu Ya Tanzania (BoT) Yatoa Tamko


SARAFU mpya ya shilingi 500 inadaiwa kuhujumiwa na baadhi ya watu ambao huinunua kwa Sh 2,500 na baadaye kuiyeyusha kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha (silver).

Vurugu Burundi: Mitandao ya Kijamii Ikiwemo Facebook,Twitter,Whatsapp Yafungwa


MAMLAKA nchini Burundi zimekata mawasiliano ya mitandao ya kijamii kupitia simu za mkononi, ambayo yamekuwa yakitumika kupanga maandamano ya kumpinga Rais Pierre Nkurunziza.

IRAQ: Wapiganaji 91 wa Kundi la Dola la Kiislamu (IS) Wauawa


WAPIGANAJI 91 wa kundi la Dola la Kiislamu (IS) wameuawa na jeshi la Iraq lililokuwa likisaidiana na wapiganaji wa kujitolea katika sehemu mbalimbali huko nchini Iraq.

aasisi Ya Kiislam Yatishia Kuandamana Nchi Nzima......Yaipa Serikali Siku 15 Kufungua Madrasa na Kuwaachia Huru Masheikh Waliokamatwa

T


Jumuiya na Taasisi za Kiisalam nchini, imetoa tamko na kuipa serikali siku 15 kabla ya kufanya maandamano nchi nzima kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakidai kufunguliwa kwa madrasa zilizofungiwa kwa kuhusishwa na kutoa mafunzo ya ugaidi.

Jumatano, 29 Aprili 2015

UKAWA Washindwa Kuafikiana.......NCCR Mageuzi Yawasilisha Hoja Ya Kujitoa, CUF Watoa Masharti Mazito


KIKAO cha viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimeshindwa kuendelea baada ya baadhi ya wajumbe kushindwa kuafikiana kuhusu hoja iliyowasilishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi, ya kutaka kujitoa kwenye umoja huo, imefahamika.

UKAWA Washindwa Kuafikiana.......NCCR Mageuzi Yawasilisha Hoja Ya Kujitoa, CUF Watoa Masharti Mazito


KIKAO cha viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimeshindwa kuendelea baada ya baadhi ya wajumbe kushindwa kuafikiana kuhusu hoja iliyowasilishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi, ya kutaka kujitoa kwenye umoja huo, imefahamika.

Mahakama Kuu Kenya Yakubali Ombi La Vyama Vya Mashoga Kusajiliwa


Katika hatua ya kushitua, Mahakama Kuu nchini Kenya imesalimu amri mbele ya mashinikizo ya watetezi wa vitendo vichafu vya ulawiti,

Rais Kikwete Akutana na Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton jijini Dar es Salaam


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam jana April 29, 2015.

Rais Kikwete Azindua Meli Mbili Za KIVITA Kwa Kishindo Jijini Dar


RAIS Jakaya Kikwete, jana amezindua na kuzitunukia Kamisheni meli mbili za kivita za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kamandi ya Wanamaji ambazo zitatumika kufanya doria na kulinda mipaka ya majini katika Bahari ya Hindi.

Godbless Lema Amshambulia Zitto Kabwe......Amtuhumu Kuikosesha CHADEMA Ushindi Mwaka 2010


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewatoa hofu wanachama wake mkoani Shinyanga kikidai propaganda zinazoenezwa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, anayedai chama hicho kimepoteza mwelekeo si za kweli bali ni uongo.

Jumanne, 28 Aprili 2015

MAGAZETI LEO JUMATANO TAREHE 29.4. 2015

 
 

DKT. SHEIN MGENI RASMI UZINDUZI MBIO ZA MWENGE RUVUMA

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2015 ambazo Kitaifa zinafanyika Mkoani Ruvuma.Kauli hiyo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua meli mbili kubwa za kisasa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua meli mbili kubwa za kisasa za kivita zenye meta 60, mizinga mikubwa miwili na ya kawaida sita kila moja, na uwezo wa kupiga makombora umbali wa kilometa saba angani na kilometa tisa chini ambazo zitakazowezesha usalama wa

Katiba ya CHADEMA ina mapungufu - Said Arfi



Mbunge wa Mpanda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demkrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa hakubaliani na katiba ya chama chake hususani kifungu kinachomzuia mwanachama kwenda mahakamani endapo ataona hajatendewa haki ndani ya chama chake.
Mbunge wa Mpanda Mjini Said Arfi
Mbunge wa Mpanda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demkrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa hakubaliani na katiba ya chama chake hususani kifungu kinachomzuia mwanachama kwenda
mahakamani endapo ataona hajatendewa haki ndani ya chama chake.

Jee, Burundi itaweza kuepuka hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ?

Uamuzi wa chama tawala nchini Burundi wa kumteua Rais Pierre Nkurunziza kugombea tena hapo tarehe 26 Juni unaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe, 

Burundi Proteste Waandamanaji wakiwa wamekusanyika mjini Bujumbura kupinga tangazo la CNDD-FDD kumteua tena Rais Pierre Nkurunziza kugombea.
Ni ishara inayohatarisha demokrasia barani Afrika. Kulikoni katika nchi za maziwa makuu? Viongozi wanazidi kungang'ania mamlaka hawataki kuyaachia na

Wakazi Iringa jitokezeni kujiandikisha- Msigwa.


Wakazi wa mkoa wa Iringa wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mbunge wa iringa mjini Chadema Mchungaji Peter Msigwa akiongea katika moja ya mikutano ya Chama cha demokrasia na Maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini mh. Peter Msigwa amewataka wananchi kujitokeza na kuacha kuhofia foleni kwani kwa
kuacha kujiandikisha watakuwa wamejikosesha haki yao ya msingi.

Yanga waingia kambini kujiandaa na Etoile


Mabingwa wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara, Young Africans, wameingia kambini kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora dhidi ya Etoile du Sahel.
Akizungumza na East Africa Radio, mkuu wa kitengo cha mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema, wanatarajia kuondoka wakiwa na msafara wa watu 50 kukiwa na viongozi, wachezaji na benchi la ufundi wakiwa sambamba na mashabiki watakaokuwa wakiwapa sapoti katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii nchini Tunisia.
Muro amesema, mpaka sasa hakuna majeruhi katika kikosi hicho na wanaamini watafanya vizuri katika mchezo huo na hatimaye kuingia katika hatua ya nane bora hatua wanayoamini watakwenda nayo vizuri.

Dar yazizima kwa mchezo wa vifaa vya moto


Kwa mara ya kwanza hii leo jijini Dar es Salaam mashabiki wa michezo wameshuhudia mchezo wa aina yake kwa wachezaji mbalimbali kuchezea vyombo vya moto kwa mitindo na mbwembwe za aina yake nakukonga nyoyo za mashabiki waliokua wakishuhudia mchezo huo
Mmoja wa wachezaji wa mchezo wa kuchezea vyombo vya mto akichezea pikipiki
Mamia ya mashabiki wa michezo jijini Dar es Salaam hii leo walishuhudia burudani ya aina yake ya michezo ya kucheza na magari, pikipiki na viatu vya magurudumu michezo iliyofanyika katika viwanja vya

MAGAZETI LEO JUMANNE TAREHE 28.4.2O15


WAZIRI MKUU PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA TAKWIMU

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na washiriki wa Kongamano la Takwimu barani Afrika baada ya kufungua mkutano wa kwenye

YANGA BINGWA LIGI KUU YA VODACOM 2014/2015

Wachezaji wa timu ya Yanga.
YANGA SC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuifunga Polisi Morogoro mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, licha ya kuwa imesaliwa na mechi kadhaa kumaliza msimu wa 2014/2015. Wafungaji wa mabao ya Yanga leo ni Amiss Tambwe aliyefunga hat trick na Simon Msuva.
KIKOSI CHA YANGA: Dida, Abdul, Joshua, Twite, Yondani, Juma, Msuva, Niyonzima, Tambwe, Ngassa, Sherman.
KIKOSI CHA POLISI MORO: Abdul, Teru, Mganga, Abel, Kambole, Selemani, Bantu, Mkangu, Bahanuzi, Kassim, Ambrose.

CHUPA ZA BIA ZAIDI YA MAMILIONI ZINATEGEMEWA KUUZWA USIKU WA PAMBANO

27F5B34500000578-3057193-image-a-52_1430126146849
Malori ya kutosha yameshafikisha mamilioni ya bia maarufu kama Budweiser, Miller Lite, Corona na Tecate kwenye hotel ya MGM Grand ambapo pambabo la

Tanzania na Norway kukarabati mradi wa umeme mtera

Tanzania na Norway kwa pamoja zinashirikiana katika utekelezaji wa mradi wa umeme kukarabati mitambo ya Kidatu na Mtera ili kuwa na upatikanaji wa uhakika wa umeme
.
Hayo yameelezwa na maafisa wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wakati waandishi wa habari walipotembelea mitambo hiyo na kuelezwa kuwa mabwawa ya mitambo ya Kidatu na Mtera yalikuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya ufuaji umeme.

Muswada wa Sheria ya Mtandao 2015 : Ikulu Yasema Hauna Tatizo Lolote…


Ikulu imesema Rais Jakaya Kikwete atasaini Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, kwa kuwa umepitia taratibu zote. Pia, Ikulu imesisitiza kuwa sheria hiyo ni nzuri na itadhibiti matumizi mabaya ya mtandao.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alitoa taarifa hiyo jana, alipozungumza na waandishi wa habari, Ikulu jijini Dar es Salaam. Rweyemamu alisema sheria ya Makosa ya

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi


Mnamo tarehe 24/4/2015 huko maeneo ya Sogea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, METHEUS ANGANILE MWAFONGO, Mndali, 37yrs, Mkuu wa Ulinzi CDM Wilaya Momba, pamoja SALEHE TABLEI@SICHALWE, 22yrs, mkazi wa Majengo Tunduma walikamatwa kutokana na taarifa za kiintelijensia.

Jumanne, 21 Aprili 2015

Natangaza ‘TOKOMEZA MBATIA VUNJO’ na ninasema nipo fiti - Mrema


Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema akiongoza maandamano ya wakazi wa Kijiji cha Lole, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ikiwa ni sghemeu ya ziara yake jimboni humo juzi.

Majambazi yavamia gari Moshi na kuua




Taarifa kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro zinazema kuwa majambazi yamevamia gari dogo aina ya Hiace lililokuwa limebeba fedha, mali ya Bonite Bottlers na kuwaua dereva na mlinzi wa kampuni kwa kupiga risasi na kisha kutoweka na fedha.

Raia afanikisha kuzuia waliopora na kujaribu kutimua


Jumapili, 19 Aprili 2015

Zitto Kabwe akanusha tuhuma dhidi ya Dk. Mengi...Asema wanaomhusisha ni walioumbuliwa na PAC


Siku moja tu baada ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, kutangaza usalama wa maisha yake kuwa hatarini, kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameibuka na kudai tuhuma alizohusishwa dhidi ya Mengi si za kweli.

Mwalimu ajinyonga, mtendaji agongwa na kufariki papo hapo


Watu wawili wamekufa mkoani Mara katika matukio mawili tofauti. 
 
Akizungumzia matukio hayo Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Audax Mjaliwa alisema katika Mtaa wa Nyamatare Manispaa ya Musoma, mwalimu Tengeru Mongu (43) wa Shule ya Msingi Igina wilayani Serengeti alikutwa amejinyonga katika chumba cha binamu yake Mauma Machunde.

Watanzania Washika Silaha Afrika Kusini....Wajiandaa Kujihami Dhidi ya Mashambulizi ya Wenyeji


Raia wa Tanzania wanaoishi Afrika Kusini sasa wanadaiwa kushika silaha tayari kwa mapambo dhidi ya vikundi vya raia wa Taifa hilo vinavyoshambulia wahamiaji wa Kiafrika.

Serikali Yarejesha Utaratibu wa Madereva kwenda Kusoma Kila baada ya Miaka Mitatu



Serikali imerejesha mafunzo ya madereva kila baada ya miaka mitatu wakati wa kumalizika kwa muda wa leseni zao, huku ikifafanua kuwa elimu watakayoipata ina umuhimu katika kazi zao, kutokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea katika sekta hiyo.

Ijumaa, 17 Aprili 2015

TAHADHARI KWA MADEREVA KONA HIZI ZA IYOVI NI KALI ZAIDI EPUSHA MAISHA YA ABIRIA CHUKUA TAHADHARI DHIDI YA AJALI‏


 wewe  ni  dereva  wa basi la abiria ama  gari  binafsi ?hebu  chukua  hatua ya  kupunguza ajali  leo kwa kujihadhari na  kona  hizi na Iyovi na Kitonga na  kona  nyingine kali kama  hizi nchini kwani maisha  yako ni  dhamani  kubwa na uhai  wake bado tunautamani
 Vema  kuheshimu alama  za barabarani na  kuacha mbwembwe  uwapo  barabarani katika kona kali kama hizi

Amuua mjomba wake na yeye kuuawa na wananchi wenye hasira mjini Mbeya

Amuua mjomba wake na yeye kuuawa na wananchi wenye hasira mjini Mbeya

Mtoto mwenye umri wa miaka 05 aliyetambulika kwa jina la Jonson Mwamwere, mkazi wa Nsalaga jijini Mbeya, aliuawa kwa kupigwa sululu kichwani na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili na mjomba wake aitwaye Yona Mwamwere.
Kwa Mujibu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahamed Msangi, Mwamwere alikuwa anamfukuza mtoto huyo na alikimbilia kwenye jengo lililopo jirani na nyumbani kwao ambalo bado lipo kwenye ujenzi na alipofika kwenye jengo hilo alimuua mjomba wake huyo kwa kumpiga kichwani kwa sululu na kutenganisha kichwa na kiwiliwili

BREAKING NEWS: WATU 20 WAMEFARIKI KWA KUFUNIKWA NA KIFUSI, KAHAMA


Wachimbaji madini wadogo 20 waliokuwa wakichimba katika machimbo ya dhahabu ya Kalole wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi usiku wa kuamkia leo.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali peponi
@eastafricatv

WANANCHI WAJITOLEA KUCHIMBA NGUZO KUPELEKA UMEME MANDA

Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo akichimba mashimo ya nguzo za umeme unaoelekea Manda
Katibu wa vijana wa CCM Bw.Menrad Mtega akitoka kuchimba shimo

Jumla ya Mara Iliyotazamwa