Abdulrahman
Hamis Clemensi enzi za uhai wake.JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro
linamshikilia Zamili Shabani kwa madai ya kumnyonga hadi kumuua mtoto
wake wa kambo, (mwaka mmoja na nusu) huku mauaji hayo yakihusishwa na
wivu wa mapenzi.
Tukio
hilo la ajabu lililowaacha vinywa wazi wakazi wa eneo hilo lilijiri saa 6
mchana wa Desemba 2, mwaka huu kwenye nyumba waliopanga wanandoa hao,
Zamili na mkewe, Rehema Mustafa (21) iliyopo Kijiji cha Mbogo, Tarafa ya
Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani hapa.
ALIVYOSEMA SHUHUDA
Kabla ya
kuzungumza na mama wa marehemu, Uwazi lilipata mawili-matatu kutoka kwa
shuhuda mmoja wa tukio hilo. ”Mimi moja kwa moja namlaumu mama wa mtoto,
Bi. Rehema. Awali alikuwa kwenye ndoa na mumewe Hamis, wakabahatika
kumzaa Abdulrahman.
“Mwanzoni
mwa mwaka huu alifika Zamili akitokea Zanzibar. Kwa taarifa tulizonazo
Zamili alikuwa na ishu kubwa kule ndiyo maana akaamua kuja huku. “Unajua
vijijini, mtu akitokea mjini wanawake wanamshobokea. Dada yetu Rehema
akadanganywa na Zamili akatoka kwenye ndoa yake na kuolewa naye mwezi wa
saba mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni