Sehemu ya maduka ambayo yalianzwa kujengwa hapo
Kutokana na kuvunjwa kwa mkataba huo hivi sasa Halmashauri itajengwa maduka hayo kwa gharama zake na kukodisha kwa bei kulingana na wakati husika ili kukuza mapato ya Halmashauri hiyo ambayo kipato chake ni chini zaidi
HALMASHAURI ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe yaanzakurejesha fedha zaidi ya Tsh mlioni 68 kwa wananchi wake baada ya kuvunja mkakaba kandamizi kwa uchumi wa Halmashauri huo kati yake na wananachi hao baada ya kubaini kupata hasara kubwa zaidi .
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw Wiliam Waziri ameueleza mtandao huu wa matukiodaima leo kuwa hatua ya kurejesha fedha hizo ambazo ni kiasi cha Tsh milioni 3 kwa kila mmiliki wa jengo ene hilo la uwanja wa mpira na ule wa mikutano mjini Ludewa baada ya wananchi waliokuwa wakijenga hapo kuonyesha kugeuka makubaliano ya mkataba .
Alisema kuwa kwa mujibu wa mkataba wananchi hao walipaswa kujenga kwa gharama zao na kwa kipindi cha miaka mitano wangeweza kurehjesha gharama zao kwa kulipa kodi ya nusu kodi na nusu ya kodi hiyo kuweza kuingia katika mapato ya Halmashauri na baada ya miaka mitano ya kurudisha gharama zao basi wangeingia mkataba upya kama wapangaji ambao wangeanza kulipa kodi kulingana na viwango pendekezi vya kodi ya Halmashauri.
"Tumelazimika kuvunja mkabata huo baada ya kuona wananchi wameanza kukiuka makubaliano mapema na iwapo tutaacha hivyo yawezekana Halmashauri kukosa mapato yake kama ilivyo katika maduka ya sokoni ambayo pia mkataba ulikuwa kama huu ila baadae waligeuka na kulipa kodi ya Tsh 15000 kwa mwaka "
Hivyo alisema katika kuepusha mapato kuendelea kukosekana katika Halmashauri hiyo ambayo hadi sasa haina chanzo cha uhakika cha mapato wamelazimika kuvunja mkakaba huo na kurejesha gharama walizotumia kwa kila mmoja na kuzirejesha ili zoezi la kujenga maduka hayo lifanywe na Halmashauri.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni