Mgombea
wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Kupitia tiketi ya Chama
cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Bw. Japhet Kembo akifurahia huku
akipongezwa na wanachama na wapenzi wa Chadema mara baada ya kuibuka
mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti kwa Kupata Kura 510 huku CCM wakiwa
wamepata kura 215 na NCCR kupata kura 205
Mawakala
wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Migombani
wakihesabu kura ambapo sanduku hilo ndio lilikuwa sanduku la mwisho
kuhesabiwa katika Kituo cha Kupigia kura cha Migombani ambao wakazi wa
Mtaa wa Migombani walikuwa wakisubiria matokeo
Baadhi
ya wapita njia nao ilibidi wasimame maana uchaguzi huu ulivuta hisia za
watu wengi kutokana na hali iliyoonyeshwa na wakazi wa mtaa huo kukaa
mpaka dakika za mwisho
Msimamizi
wa Uchaguzi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Migombani akitangaza
Mshindi wa Uchaguzi huo uliomalizika kwa Mgombea wa Chadema akiwa
ameibuka Mshindi kwa Kupata Kura 510 huku wapinzani wake wakiwa na Kura
215 za CCM na Kura 205 za NCCR
Wakazi wakishangilia kwa Ushindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni