Winnie Mandela (picha: DailyMail.co.uk) |
Kwa kipindi cha miezi miwili, Winnie Mandela, amekuwa akijaribu kupata miliki ya makazi ya Nelson Mandela katika kijiji kidogo cha Qunu, bila mafanikio.
Watu hao wanaohusika na kugawa mirathi ya Nelson Mandela, wamebaini kwamba watapinga kwa vyovyote vile ombi la Winnie Mandela la kutaka apate umiliki wa makazi hayo.
Winnie Mandela, aliishi na Mandela katika ndoa kwa kipindi cha miaka 38, lakini hakuwekwa kwenye orodha ya watu wanaopaswa kupewa mirathi ya rais huyo. Winnie Mandela, anadhani kuwa makazi ya Qunu ni milki yake, kwani Mandela aliipata wakiwa pamoja katika ndoa.
Hata hivyo wanaohusika na kugawa mirathi ya Nelson Mandela wamesisitiza kuwa makazi ya Qunu ni milki ya mke wa tatu wa Madiba, Graça Machel na kwamba jaribio lolote la marekebisho ya maandiko ya Madiba ni kinyume na kauli yake. Licha ya kukosolewa, Winnie Mandela ameendelea kuonesha kuwa yeye ndiye mwenye haki ya kumiliki mali ya Mandela, hususan makazi yake ya Qunu.
Winnie amefungua mashitaka kwenye Mahakama Kuu ya Mthatha, nchini Afrika Kusini. Amekosoa vikali ni kwa nini Mandela alimpa Graça makazi ya Qunu wakati ambapo ana nusu ya uraia wa Msumbiji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni